Header Ads Widget

MBOWE APEWA ONYO KILIMANJARO

Mgombea Ubunge jimbo la Hai kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limetoa onyo kwa mgombea Ubunge jimbo la Hai kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, baada ya mgombea huyo kutaka kufanya mkutano siku ya jana mahali ambapo hakutakiwa kuwepo.

Akizungumza hii leo Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Emmanuel Lukula, amesema kitendo hicho si sahihi na kuwataka baadhi ya wagombea kuheshimu sheria, Kanuni, taratibu zilizowekwa na Tume ya uchaguzi.

''Mgombea wa CHADEMA wilaya ya Hai alitaka kufanya mkutano mahali ambapo hakupaswa kuwa pale lakini Polisi tulimuelimisha lakini pia tukamtaka asifanye hivyo,yeye kwenye eneo hilo amepangiwa kufanya mkutano tarehe Oktoba 14'' amesema Kamanda Lukula

''Kama jana angefanya mkutano lakini kijiji jirani na nadhani ndio njia ya kupita walikuwepo wenzao wa Chama cha Mapinduzi watu wana mihemko tofauti tofauti mnaweza mkafanyiana fujo polisi tukaingia kwenye kazi nyingine'' ameongeza Kamanda Lukula

Aidha ametoa wito kwa wagombea kwa ngazi yoyote ile kuheshimu miongozo ya Tume ya uchaguzi ambapo amesema inarahisisha kazi ya ulinzi na usalama.

Post a Comment

0 Comments