Header Ads Widget

WAGANGA WAWILI WA KIENYEJI WAHUKUMIWA MIAKA MIWILI JELA KWA KUOMBA RUSHWA YA SH 500,000MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wilaya ya Babati imewahukumu kifungo cha miaka miwili jela waganga wawili wa kienyeji, Luhanga Mindi Mabeshi na Hamisi Juma Gambona baada ya kuwakuta na hatia ya kuomba rushwa ya Sh Laki Tano (500,000) na kupokea Sh 200,000 kinyume na kifungu cha 15 cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Soma zaidi taarifa iliyotolewa leo Septemba 10, 2020 na Mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara, Holle Makungu