Header Ads Widget

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA AAGIZA KUSITISHWA UTOAJI WA LESENI UCHIMBAJI MAKAA YA MAWENa Eliud Rwechungura – Wizara ya Viwanda na biashara

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa amemuagiza katibu Mkuu wa wizara ya viwanda na Biashra Prof. Riziki Shemdoe kusitisha utoaji leseni mpya ya uchimbaji wa makaa ya mawe kwa kampuni ya TANCOAL ENERGY LIMITED na ameagiza timu maalum kuchunguza mikataba iliyowekwa kati ya kampuni ya TANCOAL ENERGY LIMITED na Serikali kupitia taasisi ya NDC.

Bashungwa ametoa maagizo hayo August 03, 2020 alipotembelea na kukagua mradi wa uchimbaji wa makaa ya mawe katika mgodi wa Ngaka uliopo eneo la Ruanda wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma.

Bashungwa amefikia maamuzi hayo baada ya kampuni ya Tancoal Energy Limited kushindwa kulipa gawilo la serikali la kiasi cha Shilingi Bilioni 2.7 ambazo ni asilimia 30 ya umiliki wa mgodi wa Ngaka.

Makaa ya mawe bora yabaki ardhini kuliko kuchibwa lakini serikali hainufaiki na Chochote, ili tukipata wabia wazuri ambao wapo tiali kutoa sitahiki za nchi kulingana na mikataba iliyowekwa ili mwekezaji apate asilimia zake pia sisi kama serikali tupate sehemu yetu” amesema Bashungwa.

Aidha, Bashungwa ameagiza timu maalum iliyoundwa kuanza kazi mara moja ya kuchunguza na kufatilia mikataba iliyosaniwa toka awali uchimbaji ulipoanza mpaka sasa ili kama mikata ni mibovu iweze kurekebishwa ili Serikali kupitia Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) lipate hisa ambayo ni asilimia 30 za umiliki wa mgodi huo.

Tume maalum iliyoundwa kwa kushirikiana na Katibu Mkuu, chukueni mkataba wa Tancoal uwekeni kwenye mzani kwa kutumia sheria ili kama kuna mikataba mibovu haitufai, tuanze upya na hisa ambazo tunasitahili kuzipata, tuzipate maana hatumezi kuwa na taasisi ya NDC yenye rasilimali nyingi lakini ni masikini ya kutupa” amesema Bashungwa

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Prof. Damian Gabagambi ameeleza kuwa mpaka sasa shirika linadai kampuni ya Tancoal kiasi cha Shilingi bilioni 2.7 ambazo ni gawio la asilimia 30 za umiliki wa mgodi huo kwa serikali ambalo hawajalipa kwa miaka minne mfurulizo.