Header Ads Widget

SIMBA QUEENS KUKABIDHIWA UBINGWA AGOSTI 12 NYAMAGANA, MWANZA

      Kikosi cha Simba Queens

TIMU ya Soka ya Wanawake ya Simba, Simba Queens ambayo jana Agosti 5, 2020 ilitwaa rasmi ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara (SerengetiLite Women Premium League) - SWPL, inatarajiwa kukabidhiwa taji la ubingwa huo katika Uwanja wa Nyamagana, Mwanza katika mchezo wake wa mwisho wa ligi hiyo dhidi ya timu ya TSC Queens ya Mwanza.

Sherehe hizo za kukabidhiwa ubingwa zitafanyika Agosti 12, 2020 jijini Mwanza.