Header Ads Widget

MKANDARASI WA MAJI SHINYANGA APEWA MIEZI 2 KUUKABIDHI MRADI



Waziri wa maji Profesa Makame Mbarawa akiangalia namna mabomba yatakayopeleka Maji Masengwa yanavyounganishwa.

Na Shinyanga Press Club Blog
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa amemuagiza Mkandarasi anayetekeleza mradi wa maji kutoka Shinyanga hadi kata ya Masengwa kukamilika kabla ya mwezi wa tisa kuisha ambapo mkataba wake utakamilika.

Profesa Mbarawa ametoa agizo wakati akikagua mradi huo  unaotekelezwa na kampuni ya Emirates builders ya jijini dar ambapo amesema kuwa umekuwa kero na kuchukua  muda mrefu pasi kukamilika na.kumtaka mkandarasi huyo kukamilisha ili wakazi wa Kata ya Masengwa na vijiji jirani viweze kunufaika na huduma ya maji safi na salama

“Ninaomba nikwambie kuwa mradi huu ukamilike kabla ya mwezi septemba kwani wananhi wamekuwa wakipata adha kubwa ya maji ili hali mradi upo hivyo iwapo utashindwa kukamilisha kwa wakati tutaleta wahandisi wa wizara watakamilisha na hutapewa kazi yoyote ndani ya wizara ya maji” amesema Mbarawa .

Aidha waziri Mbarawa amesema kuwa mradi huo umechukua muda mrefu kukamilka kutokana pamoja na fedha nyingi zaidi ya shilingi bilioni 3 kwa kusema kuwa utaratibu uliotumika kuwapata wakandarasi haukuwa sahihi ndo maana umetumia fedha nyingi  na  kutumia wakandarasi ambapo ungetumia mfumo wa akaunti ya dharura (force Account) mradi huo ungegharimu  fedha kidogo na muda mfupi.

Ninaomba nikwambie mwenyekiti wa chama cha mapinduzi siwezi kujilaumu mimi na ninyi mlishiriki kwa sababu mlikuwa sehemu ya madiwani mliopitisha mradi huu matokeo yake ni shida lakini hatutakaki kurudi nyumba kazi imefikia asilimia 84 iliyobaki ni kidogo tumekubaliana kabla ya mwezi wa tisa kuisha mradi uwe umekamilka,” amesema.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amesema kuwa  kutokana na kauli ya mkandarasi huyo  kuwa kabla ya  tarehe 27 mwezi wa tisa atakuwa amekamilisha mradi huo atahakikisha anafutailia kwa ukaribu kuona iwapo mradi umekalimika kwa viwango vinavyotakiwa.

“Naomba nikuaidi mheshimiwa waziri mimi na kamati yangu nitaendelea kufuatilia kwa ukaribu mradi huu na kumisimamia ili kuhakikihsa wakazi wa masengwa na maeneo ya jirani wanapata maji kwa wakati na kuondoa kero iliyowasumbua kwa muda wa miaka mingi,” amesema

Awali Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Edward Ngelela amesema kuwa mradi huo umekuwa ukienda taratibu kwa  takribani miaka 3 na kupelekea wananchi kuhangaika  kusaka maji na kushindwa kufanya shughuli za maendeleo.

“Mheshimiwa waziri nikuombe utusaidie mradi huu ukamilike kwa wakati ili utusadie hata siye kujieleza kwa wananchi maana kila tunapoenda kuzungumza nao kilio chao kikubwa ni maji hawana kingine zaidi ya maji,” alisema.

Hata hivyo Msimamizi wa mradi wa Shinyanga Masengwa Muhandisi Saidi Msangi toka kampuni ya Emirates amehaidi kutekeleza agizo la waziri na kusema kuwa kabla ya Septemba 27 mradi huo utakuwa umekamilka'

Aidha Waziri Mbarawa amekagua miradi inayotekelezwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Shinyanga SHUWASA katika Kata za Ngogwa na Kitwana Halmashauri ya Mji Kahama na kupongeza hatua ambayo miradi hiyo imefikia kutokana na usimamizi imara wa Mkurugenzi wa SHUWASA Bi Flaviana Kifizi ikiwemo matumizi mazuri ya fedha

Akizungumzia  ujenzi wa miradi hiyo Mkurugenzi mtendaji wa Shuwasa Flaviana Kifizi amesema kuwa wametumia  mfumo wa akaunti ya dharura na kuchangia kujenga miundombinu hiyo kwa gharama nafuu

 huku akihaidi kutekeleza kwa wakati ambapo amemuomba waziri kusaidi kuharakisha fedha za kuchimba mitaro kwa ajili ya kulaza mabomba kiasi cha zaidi ya shuilingi milioni 80 ambapo waziri mbalawa amemuhakikihsia kuwa fedha hizo zitafika kiwa wakati ndani ya wiki mbili


Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akizungumza na Wakazi wa Masengwa wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya maji 




 Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akitoa maelezo kwa Waziri wa Maji wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maji mkoani Shinyanga.


 Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Shinyanga Muhandisi Emaely Nkopi akiwa katika ziara ya  waziri wa Maji.


 Waziri wa Maji akiendelea  na ukaguzi wa miradi 


 Tanki la Ngogwa litakalohudumia zaidi ya wakazi elfu 40 


 Mojawapo ya Tanki la Maji linalojengwa kijiji cha Kitwana 


 Mkurugenzi wa Shuwasa Bi Flaviana Kifizi akiznugumza mbele ya waziri wa maji 



 Waziri wa maji profesa Mbarawa akikagua Tanki la maji Kijiji cha Masengwa
Picha zote na Shinyanga Press Club Blog