Header Ads Widget

DHAMANA NI HAKI YA MTUHUMIWA, ACP DEBORA MAGILIGIMBA RPC SHINYANGA

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Shinyanga , Debora Magiligimba  alipokuwa akiongea na wananchi wa wilaya ya Kahama katika mkutano wa hadhala wa kusikiliza kero zao uliofanyika kwenye uwanja wa shirika la nyumba mjini Kahama.

Na Patrick Mabula Kahama

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Shinyanga ,Debora Magiligimba amesema dhamana hi haki ya kila mtu na kuwataka  wananchi wasiwe wanatoa rushwa  kwa askari polisi wanapodhamini  ndugu zao kwa sababu n kisheri.

Akiongea na wananchi  kwenye mkutano wa hadhala juzi mjini Kahama alisema  pia katika swala la kutoa dhamana nae askari polisi nao hawatakiwi  kuomba rushwa kwa mtu yeyote anayetaka dhamana kwa mjibu wa sheria.

Magiligimba alisema askali polisi yeyote  hatakiwi kuomba rushwa kwa mwananchi yeyote anateka dhamana kwa ndugu na jamaa yake kwa sababu kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na ni kosa ndani ya jeshi la polisi.

Alisema mwananchi yeyote atakayenyimwa dhamana au kutoridhika na huduma aliyopewa  na askari aliwataka kuwaona viongozi  polisi wa ngazi ya juu na kutoa taarifa yao kwa atakayotendewa pamoja na swala la kuombwa rushwa.

Magilingimba alisema kwa upande wao nao wananchi wasiwe chanzo cha kuwashawishi askali polisi kupokea rushwa katika kuwahudumia  kwa sababu kufanya hivyo ni kosa la kisheria na kuwataka kutojihusisha na vitendo hivyo.

Kamanda Magiligimba alisema jeshi la polisi limejipanga kutoa huduma bora kwa wananchi na kuwataka wajikite katika kutoa taarifa za kuzuia  uharifu mapema badala ya kusubiri ufanyike ndiyo watoe ripoti  kituo cha polisi.

Aidha katika mkutano huo alitoa onyo kari kwa jamii  kuacha mara moja kitendo cha kuwa wanajichukulia sheria mkononi cha kuwa  wanaua watu wanapowakamata  kwa tuhuma mbalimbali  kwa sababu kufanya hivyo ni kosa kisheria na kuwataka wawe wanawapeleka kituo cha polisi au kwenye ofisi za serikali za mitaa , vijiji , kitongoji.

Kwa upande wao wananchi waliofika kutoa  malalamiko na kero yao walisema bado kunavitendo vya rushwa kwa baadhi ya askali polisi ,hasa pale  wanapotaka kuwadhamini ndugu na jamaa zao pamoja na  swala la kuwababika kesi kwa watu.

Mmoja wa wananchi hao Donarld Masele alisema kilio chake ni askali polisi walipomkamata kwa  kosa la kubambikwa na mtendaji wa kata ya Majengo mjini Kahama  kisha kumfikisha kituoni  walimnyimwa dhama licha ya kwaona viongozi wa juu wa polisi .

Akijibu hoja hizo kamanda Magiligimba alisema malalamiko na kero zote za  wananchi walizotoa katika  mkutano huo atazifanyia kazi , kwa sababu jeshi la polisi limejipanga kutoa huduma bora kwa jamii na kuwaomba waendelee kutoa ushirikiano katika kupambana na vitendo vya uharifu na rushwa ndani ya jeshi.

Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga ACP Debora Magiligimba akiwaasa wananchi wa mji wa Kahama kuacha kujihusisha na matendo maovu.

 Mwananchi wa mtaa wa Majengo mjini Kahama Donarld Masele  aliyesimama kulia alipokuwa akitoa kelo na malalamiko yake mbele ya kamanda wa polisi wa mkoa wa Shinyanga Debora Magiligimba

 Kamanda wa Polisi,Mkoani Shinyanga ACP Debora Magiligimba akiwa na kamati yake ya usalama