Header Ads Widget

WAZIRI MKUU AREJESHA FOMU, WAITARA, MISS TANZANIA NAO WAJITOSA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikabidhiwa  fomu za kuwania tena ubunge wa jimbo la Ruangwa na Katibu wa CCM wa wilaya  ya Ruangwa, Barnabas Essau kwenye Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo, Julai 15, 2020. Kushoto ni mkewe Mary Majaliwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu baada ya kurejesha fomu za kuwania tena Ubunge wa Jimbo la Ruangwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha fomu za kuwania tena Ubunge wa Jimbo la Ruangwa baada ya kuzichukua, kuzijaza na kuzirejesha. Kushoto ni Mkewe Mary Majaliwa.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za Mitaa Tamisemi,Mwita Mwikwabe Waitara amechukua Fomu za kugombea Ubunge ndani ya Jimbo la Tarime Vijijini  ili kumung'oa John Heche.

Mwita Waitara ametaja sababu zinazo msukuma  kwenda  kugombea jimbo la Tarime na kuacha jimbo la Ukonga Jijini Dar es Salaam na kutaka kugombea Tarime kwa sababu ni nyumbani  alipozaliwa na kuwa hiyo ni adhima yake tangu hapo nyuma.
Miss Tanzania mwaka 2014, Lilian Kamazima amechukua fomu ya kugombea Ubunge wa viti maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Mkoa wa Arusha.

CREDIT: MUUNGWANA BLOG