Header Ads Widget

WANANCHI 15,000 VIJIJI VYA MANDERA NA MAGOLE KILOSA WANUFAIKA NA MRADI WA MAJI

Matenki ya maji yaliyojengwa na Mradi wa Maji wa WARIDI unaotekelezwa na Winrock International kwa msaada wa Watu wa Marekani katika vijiji vya Mandera na Magole A na B Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.

Na Mwandishi Wetu
Jumla ya wananchi 15,000 kutoka vijiji vya Mandera, Magole A na B Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro wamenufaika na mradi wa maji unaotekelezwa na Shirika la Winrock International chini ya mradi maji wa WARIDI.

Hayo yamebainishwa na Mhandisi kutoka Shirika la Winrock International Zeidia John wakati  akitoa taarifa ya mradi wa maji uliotekelezwa na Shirika hilo Wilayani Kilosa.

Zeidia ameongeza kuwa Shirika hilo inashirikiana na Serikali inatekeleza mradi wa WARIDI kwa ufadhili wa Watu wa Marekani ambapo umeshanufaisha wananchi wilayani humo.
 Kaimu Mkurugenzi Msaidizi - Usajili Charles Mpaka (kulia) akiongozana na Maafisa wengine kutoka Ofisi ya Msajili wa NGOs chini ya Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii wakiangalia mradi wa ufugaji wa samaki katika kijiji cha Magua, wilayani Kilosa mkoani Morogoro  unaofadhiliwa na World Vision Tanzania.

Akizungumza katika Kijiji cha Mandera Mtendaji wa Kijiji hicho, Gladness Ntabwene amesema kuwa kabla ya mradi huo kuwepo jumla ya wananchi 5,293 kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2012 walikuwa wanapata maji kijiji hapo.

Ameeleza kuwa mpaka sasa jumla ya wananchi 6,300 wamenufaikia na mradi huo katika kijiji chake na kusaidia kupunguza changamoto ya uhaba wa maji kwa asilimia 80.

Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Ofisi ya Msajili wa NGOs iliyo chimi ya Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Timothy Mgonja amelipongeza Shirika la Winrock International kwa kusaidiana na Serikali kutatua changamoto katika jamii hasa changamoto za maji katika maeneo mbalimbali.

"Niwapongeze Shirika na wananchi kwa pamoja kwa kutekeleza mradi huu hakika tumeuona na tumejionea kwa macho kilichofanyika" alisema

Kwa upande wake Mtendaji wa kijiji cha Mandera, Gladness Ntabwene amesema jumla ya wananchi 6,300 wamaenuaika na mradi wa  maji safi na salama uliotekelezwa na Shirika la Winrock International kwaufadhili wa watu wa Marekani.

Mmoja wa wanufaika wa Mradi huo, Sikuzani Shaban amushukuru uongozi wa kijiji, wilaya na mkoa kwa kuwaruhusu wafadhili hao kuleta mradi kijiji hapo na kutatua changamoto za upatikanaji wa maji.

Naye Mjumbe wa Kamati ya Maji ya Kijiji hicho, Hamza Saleh amesema kuwa wananchi wameshiriki kwa ukaribu katika kuchimba mitalo na kufukia mabomba ya maji hivyo kuufanya mradi kuwa na wananchi katika kuulinda ili hudumu kwa muda mrefu.
Mhandisi kutoka Shirika la Winrock International, Zeidia John (kulia) akifafanua jambo kwa Maafisa kutoka Ofisi ya Msajili wa NGOs chini ya Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii walipotembelea kukagua miradi inayotekelezwa mkoani Morogoro.
Mtendaji wa Kijiji cha Mandera, Gladness Ntabwene (wa pili kulia) akifafanua jambo kwa Maafisa kutoka Ofisi ya Msajili wa NGOs chini ya Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii wakati walipotembelea kukaua miradi inatekelezwa na NGOs mkoani Morogoro.
Mhandisi kutoka Shirika la Winrock International Zeidia John (kulia) akieleza jambo kuhusu mradi wa maji wa Waridi unaotekelezwa katika Wilaya ya Kilosa kwa Maafisa kutoka Ofisi ya Msajili wa NGOs chini ya Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii.
Muonekano wa Zahanati ya Magua iliyopo Wilayani Kilosa MKoani Morogoro iliyojengwa kwa ufadhili wa World Vision Tanzania.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiiano Serikalini WAMJW