Header Ads Widget

TFF NAYO YAMSHUKIA KOCHA WA YANGA, YAAHIDI KUMSHTAKI FIFA


Luc Eymael

Na Damian Masyenene
MAMBO yamezidi kumuendea kombo aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Mbelgiji Luc Eymael baada ya Klabu yake leo mapema asubuhi kusitisha mkataba na kumfuta kazi, hatimaye masaa machache Shirikisho la Soka Nchini (TFF) nalo limeahidi kumchukulia hatua za kinidhamu kocha huyo.

Luc anadaiwa kutoa matamshi ya kashfa kwa mamlaka za soka nchini, Serikali, Mashabiki na wapenzi wa soka hususan wa timu ya Yanga yanayodaiwa kuwa ya kibaguzi na yasiyo ya kiungwana.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Julai 27, 2020 na Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Cliford Ndimbo imesema watalifikishia Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) taarifa za Kocha Luc juu ya kauli zake za kibaguzi ili nalo limchukulie hatua.