Header Ads Widget

TANESCO SHINYANGA YATOA ELIMU MATUMIZI YA UMEME KWA WACHIMBAJI MWAKITOLYO NA WENYE MASHINE ZA KUSAGA SALAWE NA SOLWA

Meneja Masoko wa TANESCO makao makuu, Monica Masawe akitoa elimu ya usalama katika matumizi ya umeme kwa wachimbaji wadogo wa madini Mwakitolyo eneo la Nyaligongo namba1.

Na Marco Maduhu Shinyanga
KATIKA kuhakikisha kwamba wateja wake hawaathiriki na matumizi makubwa ya nishati ya umeme inayowaletea usumbufu katika kulipa ankara, Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Mkoa wa Shinyanga limewatembelea na kutoa elimu ya usalama katika matumizi ya umeme kwa wachimbaji wadogo wa Dhahabu Mwakitolyo na wamiliki wa mashine za kusaga na kukoboa nafaka Salawe na Solwa wilayani Shinyanga.

Ambapo limewaasa kuacha kununua vifaa vya kusukuma mashine na Makarasha ya kusagia mawe yenye Dhahabu (Motor) vyenye uwezo mdogo vinavyowasababishia matumizi makubwa ya umeme.

Zoezi la utoaji elimu hiyo limefanyika kwa muda wa siku mbili, kwa lengo la kutoa elimu ya usalama na matumizi bora ya umeme, ili kuwaepusha na gharama zisizo la lazima kwa mtumiaji.

Akizungumza wakati wa utoaji elimu hiyo Mhandisi mtafiti Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kutoka makao makuu Aurea Bigirwamungu, amesema wametoa elimu kwa wamiliki hao wa mashine na wachimbaji wadogo wa madini, ili kuhakikisha usalama wa umeme na matumizi bora ya nishati katika kazi zao za uzalishaji.

"Tumekuja kutoa elimu kwenu ya usalama wa umeme na matumizi bora ya nishati, mara baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwenu kuwa mnatumia gharama kubwa za umeme, ambapo tumegundua motor mnazotumia zina uwezo mdogo, na hivyo kusababisha matumizi makubwa ya umeme," amesema Bigirwamungu.

"Mbinu ambayo ninawapa ili kukwepa matumizi makubwa ya umeme, ni kuacha kununua motor zenye uwezo mdogo, pamoja na kuacha kuzifanyia matengenezo zaidi ya mara mbili, bali mnunue mpya tena zenye ubora zaidi bila ya kujali bei na siyo kununua feki," ameongeza.

Naye Meneja Masoko wa TANESCO makao makuu, Monica Masawe, ametoa wito kwao kuacha kufunga mfumo wa umeme (Wiring) kwa kutumia mafundi wa mitaani, ambao siyo wataalam na wanaweza kusababisha jengo kuungua moto.

Kwa upande wake Afisa Mahusiano na Huduma kwa Wateja Tanesco-Shinyanga, Sara Libogoma amewataka wateja hao pale wanapopatwa na changamoto za umeme, wawasiliane na Shirika hilo mapema iwezekanavyo kupitia ofisi ndogo zilizopo karibu na maeneo yao, ili wapatiwe ufumbuzi wa haraka.

Nao baadhi ya wateja hao wa Tanesco walishukuru kwa elimu hiyo na kuomba iendelee kutolewa mara kwa mara ili waepukane na matumizi yasiyo ya lazima ya kuongeza gharama za umeme, hali ambayo itaongeza pato lao binafsi na taifa kwa ujumla.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mhandisi mtafiti Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kutoka makao makuu, Aurea Bigirwamungu, akitoa elimu ya matumizi bora ya umeme kwa wachimbaji wa madini ya dhahabu Mwakitolyo.
Mhandisi mtafiti Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kutoka makao makuu, Aurea Bigirwamungu, akitoa elimu ya matumizi bora ya umeme kwa wamiliki wa mashine za kusaga na kukoboa nafaka Salawe.
Mhandisi mtafiti Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutoka makao makuu, Aurea Bigirwamungu, akitoa elimu ya matumizi bora ya umeme kwa wamiliki wa mashine za kusaga na kukoboa nafaka Solwa.
Meneja Masoko wa Tanesco makao makuu, Monica Masawe akitoa elimu ya usalama katika matumizi ya umeme kwa wachimbaji wadogo wa madini Mwakitolyo eneo la Nyaligongo namba 2.
Meneja Masoko Tanesco makao makuu, Monica Masawe akitoa elimu kwa wamiliki wa mshine za kusaga na kukoboa nafaka- Salawe juu ya gharama za umeme.
Afisa Mahusiano na Huduma kwa Wateja Tanesco Mkoa wa Shinyanga, Sara Libogoma, akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu Mwakitolyo na kuwataka pale penye changamoto za umeme watoe taarifa kwa Shirika hilo kupitia ofisi ndogo zilizopo maeneo yao.
Wachimbaji wadogo wa madini ya Dhahabu Mwakitolyo wakisilikiza elimu ya usalama na matumizi bora ya umeme kutoka kwa maofisa wa Tanesco.
Wachimbaji wadogo wa Dhahabu Mwakitolyo wakisilikiza elimu ya usalama na matumizi bora ya umeme kutoka kwa maofisa wa Tanesco.
Wachimbaji wadogo wa Dhahabu Mwakitolyo wakisilikiza elimu ya usalama na matumizi bora ya umeme kutoka kwa maofisa wa Tanesco.
Wachimbaji wadogo wa Dhahabu Mwakitolyo wakisilikiza elimu ya usalama na matumizi bora ya umeme kutoka kwa maofisa wa Tanesco.
Wachimbaji wadogo wa Dhahabu Mwakitolyo wakisilikiza elimu ya usalama na matumizi bora ya umeme kutoka kwa maofisa wa Tanesco.
Wamiliki wa mashine za kusaga na kukoboa nafaka kutoka Salawe, wakiwa na maofisa wa Tanesco katika utoaji elimu ya usalama na matumizi bora ya umeme.
Mhandisi mtafiti Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kutoka makao makuu Aurea Bigirwamungu, (kulia), akitoa maelekezo kwa mmiliki wa mashine ya kusaga na kukoboa nafaka Richard Machibya (katikati) juu ya kununua Motor zenye uwezo mzuri ambazo zitasukuma mashine na kuondokana na matumuzi makubwa ya umeme.
Mhandisi mtafiti Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kutoka makao makuu Aurea Bigirwamungu, akitazama Motor ya kusukuma mashine ya kusaga na kukoboa nafaka.
Muonekano wa Motor ambazo zinatumika kusukuma mashine.

Picha na Marco Maduhu