Header Ads Widget

SIMBA KUKABIDHIWA KOMBE LA VPL JULAI 8 MKOANI LINDI





Na Damian Masyenene Shinyanga Press Club Blog

Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) imesema kuwa sherehe za kukabidhi kombe la ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) kwa klabu ya Simba SC zitafanyika Julai 8, 2020 mjini Ruangwa mkoani Lindi katika Uwanja wa Majaliwa kwenye mchezo wa ligi hiyo dhidi ya wenyeji wake, Namungo FC.

Kwa mujibu wa Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Julai 1, 2020 na Idara ya Habari na Mawasiliano ya Bodi hiyo imesema kuwa sherehe za kukabidhi kombe hilo zitafanyika mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo namba 340.

Hii sasa itakuwa ni mara ya pili mfululizo kwa mabingwa hao wa ligi kukabidhiwa kombe hilo nje ya Jiji la Dar es Salaam, ambapo msimu uliopita walikabidhiwa mkoani Morogoro katika Uwanja wa Jamhuri baada ya mchezo wao wa mwisho wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar ya Manungu mkoani humo.

Soma zaidi taarifa iliyotolewa na TPLB