Header Ads Widget

SALOME MAKAMBA APETA KURA ZA MAONI UBUNGE SHINYANGA MJINISalome Makamba akizungumza na wanachama baada ya kushinda kura za maoni

Na Marco Maduhu -Shinyanga
Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mwaka 2015, Salome Makamba, ameshinda kwenye kura za maoni ndani ya chama hicho, kugombea ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Zoezi la upigaji kura hizo limefayika leo Julai 15, 2020 kwenye ukumbi wa hoteli ya Ibanza, na kuhudhuliwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho, ambapo walipiga kura za maoni za kumchangua mgombea ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini, pamoja na Mbunge wa Viti maalum.


Aidha katika kura 177 zilizopigwa za ubunge, Salome Makamba, amepata ushindi wa kura 75, akifuatiwa na Samsoni Ngwagi kura 51, Emmanuel Ntobi kura 27, Paul Kaunda kura 10, Nicolaus Luhende kura Nane, pamoja na Obed Jilala kura Tano.

Kwa nafasi ya ubunge wa vitimaalum ambapo zilipigwa kura 58, Salome Makamba alipata ushindi tena wa kura 24, ambapo wagombea wawili aliokuwa akishindana nao ambao ni Zena Gulam na Zainab Heli walifungana kwa kupata kura 17 kila mmoja.

Aidha msimamizi wa uchaguzi huo, Peter Shio ambaye ni mwenyekiti wa chadema mkoa wa Simiyu, amesema majina ya wagombea hao yatapelekwa kwenye kamati kuu ya Chadema, ambapo wao ndio watakuwa waamuzi wa mwisho wa kupitisha jina rasmi la mgombea ambaye atagombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini.

Kwa upande wake Salome Makamba akizungumza mara baada ya kupata ushindi huo, amewataka wana Chadema kuvunja makundi yaliyokuwapo wakati wa kampeni za kugombea kwenye kura hizo za maoni, na kuwataka kuwa kitu kimoja jambo ambalo litawapatia ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi huo mkuu wa udiwani, ubunge na urais.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Salome Makamba akizungumza mara baada ya kupata ushindi wa kura za maoni kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga mjini kupitia Chadema.
Salome Makamba akiomba wajumbe kuvunja makundi na kuwa kitu kimoja ili kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu,
Awali wagombea wakisubili matokeo ya kuchaguliwa kwenye kura za maoni kupeperusha bendera ya Chadema kugombea ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini.
Wajumbe wakiwa kwenye uchaguzi.
  Wajumbe wakifuatilia kikao

Wajumbe wakiwa kwenye uchaguzi.

Picha na Marco Maduhu