Header Ads Widget

RAIS MAGUFULI AMTEUA ACP ADVERA BULIMBA KUWA DC NZEGA, WAZIRI MKUCHIKA NAYE AFANYA UTEUZI


ACP, Advera Bulimba

LEO Julai 9, 2020 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli amemteua Kamanda wa Kikosi cha Polisi TAZARA, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Advera John Bulimba kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nzega mkoani Tabora kuchukua nafasi ya Godfrey William Ngupula.

Mbali na uteuzi wa ACP Bulimba, Rais Magufuli pia amemteua Solomon Isack Shati kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang mkoani Manayara, ambapo kabla ya uteuzi huo Bw. Shati alikuwa Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe mkoani Katavi.

Wakati huo huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kept. George Mkuchika kwa mamlaka aliyokasimiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya uteuzi wa makatibu tawala wa wilaya mbili.

Soma zaidi kuhusu uteuzi huo kupitia taarifa iliyotolewa muda mfupi uliopita na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU, Gerson Msigwa.