Header Ads Widget

NCHAMBI NAYE APETA JIMBONI KISHAPU, AZOA KURA 544 KATI YA 882



Suleiman Nchambi


Mkutano wa Maalumu wa CCM wilaya ya Kishapu wa kupiga kura za maoni kupata mwanachama wa CCM atakayegombea Ubunge Jimbo la Kishapu katika uchaguzi Mkuu mwaka 2020 uliofanyika Jumatatu Julai 20, 2020 umemalizika Julai 21,2020 saa saba usiku ambapo Suleiman Nchambi aliyekuwa anatetea kiti chake ameshinda kwa kishindo katika uchaguzi huo kwa kupata kura 544 akifuatiwa na Kishiwa Francis Kapale aliyepata kura 54 na Boniphace Butondo kura 40.

Jumla wajumbe waliotakiwa kupiga kura ni 934, wajumbe waliowapiga kura ni 882, zilizoharibika 2.
Suleimani Nchambi akiwa amebeba kura zake
Suleimani Nchambi akisaini matokeo ya uchaguzi