Header Ads Widget

MSHINDANI WA UMMY MWALIMU AJIONDOA NA KUMUOMBEA KURAWaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu

Baada ya jana Julai 20, 2020 Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa kupita bila kupingwa kwenye kura za maoni katika Jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, baada ya kuwa mgombea pekee kwenye jimbo hilo, leo Julai 21, 2020 Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameombewa kura na mshindani wake ambaye amejitoa kwenye kinyang'anyiro hicho. 


Hali hiyo inakuja baada ya Mgombea ubunge jimbo la Tanga Mjini, Chawambula Abdulnab kutaka kura zake apewe Ummy Mwalimu
 Chawambula Abdulnab

Chawambula ambaye ni mmoja wa wanaoomba kuteuliwa na CCM kugombea ubunge Jimbo la Tanga Mjini, amesimama wakati wa kujinadi na kumuombea kura mgombea mwenzake, Ummy Mwalimu na yeye kujitoa. 
CHANZO - MUUNGWANA BLOG