Header Ads Widget

VIFO 11 VILIVYOSABABISHA MAANDAMANO DHIDI YA POLISI MAREKANI


Kifo cha Mmarekani mweusi ambaye alikamatwa na polisi akiwa hana silaha lakini polisi alionekana kutumia nguvu kwa kumkaba shingo na hivyo suala la ubaguzi dhidi ya jamii ndogo ya watu weusi ikaibuka.

George Floyd, aliyekuwa na umri wa miaka 46-alikuwa anafanya kazi ya ulinzi katika mgahawa mmoja wa Minneapolis, alifuatwa na polisi ambao walikuwa wanamtafuta mshukiwa wa mashtaka ya kughushi siku ya Ijumaa Mei, 25.

Video ya dakika 10-ambayo ilipigwa na shuhuda inaonyesha Floyd akimlalamikia afisa wa polisi akisema " siwezi kuhema".

Video ya tukio hilo lilisambaa kwa watu siku hiyohiyo ikionyesha mwanamke wa kizungu nchini Marekani akiwa anajibizana na mwanaume mweusi kuhusu mbwa wake ambaye alikuwa amefunguliwa.

Kifo cha Floyd kimeweza kuibua hofu ya takwimu za mauaji ya polisi dhidi ya raia weusi nchini Marekani.
Kwa mujibu wa takwimu zilizowekwa na gazeti la Washington, watu 1014 walipigwa risasi na polisi katika taifa hilo kwa mwaka 2019, na utafiti unaonyesha kuwa wamarekani weusi ndio wahanga wakubwa.

Utafiti uliofanywa na asasi ya isiyokuwa ya kiserikali unadai kuwa katika vurugu ya polisi watu weusi wako katika hatari ya kuuwawa mara tatu zaidi ya watu weuse.

Uonevu wa Polisi umepelekea kuwepo kwa harakati za thamani ya utu wa mtu mweusi kuepo #BlackLivesMatter movement. 

Watu maarufu kama muimbaji Beyonce na mchezaji nyota wa mpira wa kikapu Lebron James wameanzisha kahamasisha kampeni hizo kwa umma.

Hawa ni baadhi ya wahanga wengi wa vifo vilivyosababishwa na maandamano dhidi ya vurugu za polisi.
https://www.bbc.com/swahili