Header Ads Widget

FACEBOOK YAFUTA MATANGAZO YA KAMPENI YA RAIS TRUMP


















Kampuni ya mtandao wa kijamii ya Facebook imeondosha mtandaoni matangazo ya kampeni ya rais Donald Trump kwa kutumia alama zilizokuwa za utawala wa kinazi wa Ujerumani.
Facebook imesema tangazo lililolengwa lilikuwa na alama ya pembe tatu nyekundu kama iliyotumika na utawala wa kinazi kuwatambua wapinzani wao kama wakomunisti.

Matangazo hayo ni sehemu ya kampeni ya Trump kwa uchaguzi wa Novemba mwaka huu.

Timu ya kampeni ya Trump imesema kuwa tangazo hilo lilikuwa linakilenga kikundi cha wanaharakati wa mrengo wa kushoto antifa, ambacho wanadai kinatumia nembo hiyo.

Facebook inadai matangazo hayo yanaenda kinyume na sera yake ya chuki ya kupangwa.

"Haturuhusu alama ambazo zina simama kwa mirengo ama makundi ya chuki, labda iwe ni kukemea jambo hilo," imeeleza Facebook

"Hiko ndicho tulichokiona kwenye tangazo hili, na popote pale alama hiyo itakapotumika tutachukua hatua kama hii," ameeleza mkuu wa sera za ulinzi wa Facebook Nathaniel Gleicher.

Matangazo hayo, ambayo yalipakiwa kwenye kurasa za mtandao wa Facebook za Trump na Makamu wake Mike Pence yalifutwa baada ya kuwa mtandaoni kwa saa 24.
CHANZO -BBC