Header Ads Widget

CHAMA CHA UPINZANI MALAWI CHAPATA USHINDI WA KIHISTORIA URAIS




Mwanga wa siasa ya Lazarus Chakwera ulifufuliwa baada ya mahakama kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwaka jana

Chama tawala nchini Malawi kimetoa wito wa kufanyika kwa uchaguzi wa tatu wa urais kwa madai kwamba uchaguzi wa duru ya pili ulikumbwa na udanganyifu na vitisho.
Chama tawala cha Democratic Progressive Party (DPP) Ijumaa kilitaka tume ya uchaguzi kutupilia mbali matokeo ambayo yalikuwa yanaendelea kuingia katika uchaguzi huo na kutaka kufanyika kwa uchaguzi wa tatu.

Katibu wa chama hicho Francis Mphepo alisema katika taarifa: "Tungependa kuangazia matukio kadhaa ambayo huenda yakatia dosari uaminifu na uadilifu wa matokeo ya ya uchaguzi wa urais."

Chama hicho kiliorodhesha vituo ambavyo kilidai wasimamizi wake walitolewa nje na kusema zaidi ya kura milioni 1.5 zimetiwa dosari.

"Hakuna shaka yoyote kwamba vitendo vya udanganyifu vitaathiri matokeo kwa namna moja au nyengine,"Mphepo alisema.

Lakini kufikia Jumamosi, Bwana Mutharika alizungumza na kusema kuwa ingawa hakubaliani na matokeo ya uchaguzi, ni imani yake kwamba nchi inastahili kusonga mbele.

Mapema hafla ya kumuapisha Lazarus Chakwera kuwa rais mpya wa Malawi imefanyika katika mji mkuu wa Lilongwe baada ya kiongozi huyo kushinda duru ya pili ya uchaguzi wa urais uliofanyika Jumanne wiki iliyopita.


Bwana Chakewera alimshinda aliyekuwa rais wa nchi hiyo Peter Mutharika kwa asilimia 58.57 ya kura katika uchaguzi wa Jumanne, tume ya uchaguzi ilitangaza usiku wa Jumamosi.

Mwezi Februari, Mahakama ya katiba nchini Malawi ilifutilia mbali ushindi wa Mutharika katika uchaguzi wa Mei 2019, kutokana na dosari zilizokumba uchaguzi huo.

J

Nchi iligawanyika vikali wiki kadhaa kuelekea uchaguzi wa marudio.

Malawi ni nchi ya kwanza Afrika kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais na kuandaa duru ya pili ambayo upinzani ukanyakua ushinda.

Kama ilivyotokea Malawi nchini Kenya upinzani ulipinga matokeo ya uchaguzi wa urais mwaka 2017 na kushinda mahakamani.

Hata hivyo mgombea wa upinzani Raila Odinga alisusia duru ya pili ya uchaguzi.


Rais mteule Lazarus Chakwera akipiga kura mapema wiki hii.

Baada ya matokeo rasmi kutangazwa usiku wa Jumamosi, Bw. Chakwera alisema ushindi wake ni "ushindi wa demokrasia na haki" na kuongeze kusema: "Roho yangu imejaa furaha."

Wafuasi wake walimiminika katika barabara za mji mkuu wa Lilongwe, kushangilia ushindi wao baadhi wakipiga honi za magari na wengine wakipiga fataki.

Ushindi huu unamaanisha nini?
Tukio hili lina umuhimu mkubwa katika historia ya siasa nchini Malawi, na linaonesha wadi kwamba mahatma na time ya uchaguzi hazikuwa tayari kushinikiza kufanya maamuzi kwa kwa maslahi ya ofisi ya rais.

Baada ya hatua hiyo Bw. Mutharika alikimbilia mahakama ya rufaa kupinga uamuzi huo lakini majaji walisimama kidete kutoa uamuzi usioegemea upande wowote.

Na sasa wananchi wamefanya uamuzi wao kwa kumemkataa katika duru ya pili ya uchaguzi.

Ushindi wa Peter Mutharika mwaka jana ulifutwa na mahakama ya katiba baada ya ushahidi kuonesha kuwa uchaguzi wa mwaka jana yalichakachuliwa.


Rais anayeondoka madarakani Peter Mutharika ameutaja uchaguzi wa Jumanne kuwa mbaya zaidi uliowahi kushuhudiwa nchini Malawi

Bwana Mutharika sasa analalamika kwamba uchaguzi huo haukuwa wa haki na huenda akawasilisha malalamishi yake mahakamani, lakini raia wa Malawi wamemchagua Lazarus Chakwera kama rais wao mpya.

Akizungumza kabla ya matokeo hayo ya Jumamosi, bwana Mutharika alisema kwamba licha ya kwamba matokeo ya uchaguzi huo ''hayakubaliki'' , ni ''matumaini kwamba raia wa taifa hilo watalisukuma mbele gurudumo la taifa hilo badala ya nyuma''.

Muhubiri huyo wa kanisa la Pentecostal na muhadhiri wa somo la theolojia atalazimika kuponya vidonda vya taifa ambalo limepitia miezi kadhaa ya msukosuko wa kisiasa.
CHANZO -BBC