Header Ads Widget

POLISI DODOMA YAKAMATA MAGARI 17 YA WIZI

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma limekamata magari 17 yadhaniwayo kuwa ya wizi katika msako wa siku nne uliofanyika kati ya tarehe 19.5.2020 hadi tarehe 22.5 2020.
Hayo yamesemwa  Mei 26,2020   na  kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kuwa walimkamata Helman Stephen akiwa na gari namba T.891 BXY Toyota PREMIO gari ambalo linatumia kadi na usajili wa kubatizwa za gari lingine huku akisema kuwa walimkamata Athuman Juma Pambagu mwenye umri wa miaka 29 mkazi wa Nzuguni mwenye gari  namba T.864 CQA TOYOTA IST  chassis imekatwa na kuungwa kibati kiingine vioo vimefutwa na kubandikwa namba nyingine ambalo limebatizwa namba na card ya gari nyingine.

Aidha amesema kuwa wamekamata gari lenye namba ya T.237 DSJ aina ya SUBARU ni gari la transit {IT} lilikuwa linasafirishwa kwenda Uganda ambalo dereva alipakia abiria wawili huko MISUGUSUGU Pwani kwenda Kahama Shinyanga ambapo dereva alitishiwa silaha na kuporwa gari na kufungwa kamba na kutupwa porini eneo la Pandambili kongwa .

Sanajari na hayo Kamanda  Muroto amesema kuwa walimkamata Festo Castory Lalika akiwa na vifaa vya pikipiki 4, jenereta mbili  na engine moja ya bajaji huku pia akikamatwa Lello Michael Ringo akiwa na Tv 3 aina ya SAMSUNG,SUBWOFER 1 Vichwa vya cherehani 2,laptop 1 HP Stabilizer 2 ambazo ni mali  za wizi na vifaa vya kuvunjia drill 1 na  panga .

Hivyo amesisitiza watu  waache kujihusisha na uhalifu wa aina yoyote ikiwa ni pamoja na wizi , na magari ya wizi wayasalimishe haraka  katika kituo cha polisi kabla ya kukamatwa huku akiwashauri watu ambao wananunua magari wahakikishe wanayakagua magari hayo kabla ya kununua ili wasiingie katika matatizo ya kumiliki chombo cha  wizi.