Header Ads Widget

AKAMATWA KWA KUVAA SARE ZA JWTZ ALIZOIBA KWA BABA MKWE ILI ASILIPE NAULI KATIKA BASI


Jeshi la Polisi mkoani Kagera, linamshikilia Mrisho Ibrahimu mwenye umri wa miaka 34 kwa tuhuma za kukutwa na sare za Jeshi la Wananchi (JWTZ), ambazo imedaiwa aliziiba kutoka katika nyumba ya Baba Mkwe wake, mkoani Arusha.

Kwa mujibu wa maelezo yake mwenyewe amesema, alichukua nguo hizo ili asilipe nauli katika basi.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi amesema kuwa kijana huyo alikamatwa akiwa katika nyumba moja ya kulala wageni, eneo la Kamachumu wilayani Muleba, na kuwa alipohojiwa amekiri kuiba sare za baba mkwe wake, ambaye ni Askari wa JWTZ mkoani Iringa, na kujifanya ni Askari wa Jeshi hilo kikosi cha mizinga mkoani Arusha.

Akieleza sababu ya kufika mkoani Kagera, Kijana Mrisho Ibrahimu amesema, alimfuata mpenzi wake wa kando (mchepuko) ambaye alimpata kupitia mitandao ya kijamii na kuwa alipofika mkoani humo hakubahatika kukutana naye, ndipo alipoanza kufanya utapeli ili apate nauli ya kurudi alipotoka
TUTUMIE HABARI,PICHA,MATUKIO AU TANGAZO LAKO TUKUWEKEE KWENYE SHINYANGA PRESS CLUB BLOG,WASILIANA NASI KWA Email : shinyapress@gmail.com Simu/WhatsApp 0756472807