Header Ads Widget

RAIS MAGUFULI ASEMA ANAFIKIRIA KUFUNGUA VYUO NA MICHEZO...ASIMULIA JINSI MWANAE ALIVYOKULA LIMAO,TANGAWIZI,KUJIFUKIZA AKAPONA CORONA


Rais Magufuli amesema kuanzia wiki ijayo kama maambukizi ya Corona yataendelea kupungua, atafikiria kufungua Vyuo na kuruhusu michezo iendelee. 

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jumapili Mei 17,2020 wakati akitoa salamu baada ya kushiriki kwenye Kanisa la KKKT Chato, mkoani Geita, ambapo atafikia uamuzi wa kurejesha michezo kwa kuwa michezo ni burudani kwa Watanzania. 

Rais Magufuli amesema kuwa "kwa trendi hii ninavyoiona kama wiki hii inayoanza kesho hali itaendelea kupungua nimepanga kufungua Vyuo ili wanafunzi waendelee kusoma, lakini pia tumepanga kuruhusu michezo iendelee."

Rais John Magufuli amesema kuwa idadi ya wagonjwa wa Corona nchini Tanzania imepungua sana, huku baadhi ya vituo vilivyotengwa kwa ajili ya kuwahudumia wenye maambukizi vikiwa vitupu.