` TAIFA GROUP YAWEZESHA WANAFUNZI WENYE MAZINGIRA MAGUMU KUPATA ELIMU KUPITIA MASHINDANO YA MBUZI

WANDAMAN HOTEL

TAIFA GROUP YAWEZESHA WANAFUNZI WENYE MAZINGIRA MAGUMU KUPATA ELIMU KUPITIA MASHINDANO YA MBUZI

     

Mkuu wa  Chapa na Mawasiliano wa  Taifa Croup,  Kemilembe Mugangala (kushoto) akikabidhiwa tuzo  ya ushindi wa Mashindano ya Mbuzi, (Goat Race  2026) na  Mtaalamu wa Masuala Endelevu kutoka Vodacom Tanzania ambao walikuwa wakuu wa wadhamini  wa 2025, nyuma kushoto ni  Makamu wa Rais wa  Rotary  Club Oysterbay,  Benoit Ducamse  na kulia nyuma ni mwanchama wa Club ya Rotary Osterbay, Shavesh Bhah.

Kutoka kushoto ni Kemilembe Mugangala, Mkuu wa Chapa na Mawasiliano wa Taifa Group; Paul Muhato, Rais wa Rotary Club ya Dar es Salaam Oysterbay; Benoit Ducarme, Makamu wa Rais wa klabu hiyo; Bhavesh Bhatt, Mjumbe wa Rotary Club ya Dar es Salaam Oysterbay; Deborah Kaluzi, Mtaalamu wa Masuala ya Foundation na Uendelevu wa Vodacom Tanzania; na Rashida Nabulime, Rais Mteule wa Rotary Club ya Dar es Salaam Oysterbay.

**

 Ushindi uliopatikana kupitia burudani sasa unageuka kuwa fursa ya kujenga maisha ya baadaye kwa watoto na vijana wa kitanzania.

Kampuni ya Taifa Group imekabidhi zawadi zake zote ilizoshinda katika Mashindano ya Mbuzi (Goat Races) yaliyofanyika mwezi Septemba  2026 kwa Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam Oysterbay, kwa ajili ya kusaidia watoto na vijana wenye mazingira magumu nchini Tanzania kupata fursa ya kuendelea na masomo ya elimu ya juu.

Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika  jijini Dar es Salaam, wakati wa mkutano wa kila wiki wa Klabu hiyo uliofanyika katika Kahawa Café, Masaki.

Zawadi hizo zilikabidhiwa na Deborah Kaluzi, Mtaalamu wa Masuala Endelevu kutoka Vodacom Tanzania, ambayo ilikuwa mdhamini mkuu wa Mashindano ya Mbuzi ya mwaka 2025.

Kwa niaba ya Taifa Group, zawadi hizo zilipokelewa na Kemilembe Mugangala, Mkuu wa Chapa na Mawasiliano.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi wa Klabu hiyo, akiwemo Bw. Paul Muhato, Rais wa Klabu ya Rotary ya Dar es Salaam Oysterbay; Bw. Benoit Ducarme, Makamu wa Rais; Bi. Rashida Nabulime, Rais Mteule; pamoja na Bw. Bhavesh Bhatt, mwanachama wa klabu hiyo.

Akizungumza baada ya kupokea zawadi hizo, Mugangala aliishukuru Vodacom Tanzania pamoja na Klabu ya Rotary kwa kuandaa jukwaa linalounganisha jamii, burudani na dhamira ya kusaidia wengine.

"Kwa niaba ya Taifa Group, tunajivunia sana kuwa sehemu ya jambo hili. Mashindano ya Mbuzi si utamaduni unaopendwa na wengi pekee, bali pia yanatukumbusha umuhimu na nguvu ya kurudisha kwa jamii," alisema.

"Kwa kuzingatia kaulimbiu ya Rotary isemayo Huduma Kabla ya Maslahi Binafsi (Service Above Self), Taifa Group imeamua kurejesha zawadi hii yote kwa jamii. Tunaamini kuwa hakuna mtoto anayepaswa kunyimwa fursa ya kupata elimu ya juu kutokana na mazingira aliyozaliwa au hali ya familia yake. Huko Taifa, hatufanyi biashara nchini Tanzania pekee, bali tunashiriki pia katika kujenga Tanzania. Ikiwa ushindi wetu unaweza kumsaidia mtoto mmoja kufikia ndoto yake ya kujiunga na chuo kikuu, basi huo ndio ushindi wa kweli",alisema.

"Kwa dhati, tunaishukuru Vodacom Tanzania kwa kuwezesha jambo hili na Rotary Oysterbay kwa kazi kubwa na nzuri mnayoendelea kuifanya kwa manufaa ya jamii zetu",alisema

Kwa upande wake, Bw. Paul Muhato, Rais wa Rotary Oysterbay, aliipongeza Taifa Group kwa uamuzi huo wa kurudisha kwa jamii, akibainisha kuwa fedha zitakazopatikana zitaelekezwa moja kwa moja katika mpango wa klabu wa kusaidia elimu  nchini.

Mashindano ya kila mwaka ya Mbuzi, yanayodhaminiwa na Vodacom Tanzania, hukutanisha kampuni mbalimbali, familia na wadau wengine kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kufanikisha shughuli mbalimbali za kijamii na misaada ya kibinadamu katika maeneo tofauti nchini.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464