` JESCA SIMUCHILE AENDELEA KUTIKISA MUZIKI WA INJILI, SASA AACHIA “NIMEMUONA BWANA”

WANDAMAN HOTEL

JESCA SIMUCHILE AENDELEA KUTIKISA MUZIKI WA INJILI, SASA AACHIA “NIMEMUONA BWANA”

   
Mwimbaji wa muziki wa Injili, Jesca Simuchile, ameendelea kuimarisha safari yake ya kuhubiri Injili kupitia muziki baada ya kuachia wimbo wake mpya unaoitwa “Nimemuona Bwana”, ukiwa na video rasmi iliyotengenezwa kwa ubora wa 4K.

Wimbo huo ni sehemu ya mwendelezo wa kazi za kimuziki za Jesca Simuchile zinazobeba ujumbe wa kiimani, matumaini, ushuhuda na kumtegemea Mungu katika maisha ya kila siku.

Kabla ya kuachia wimbo huo, Jesca alikuwa ametoa nyimbo nyingine kadhaa zikiwemo “Tuimbe Tumepona”, aliyomshirikisha Mwinjilisti Daniel Safari, uliobeba ujumbe wa ushuhuda, matumaini na kumshukuru Mungu kwa wema wake.
Aliendelea na wimbo “Neema Ingalipo”, uliosisitiza kuwa neema ya Mungu bado ipo kwa wanaomwamini na kumtumainia, huku video yake rasmi ikiwa na tafsiri za Kiingereza ili kuwezesha watu wengi zaidi kuelewa ujumbe wake.

Agosti 2026, Jesca aliachia wimbo “Ndoa Iheshimiwe”, unaobeba mafundisho ya kibiblia kuhusu umuhimu wa kuheshimu na kulinda taasisi ya ndoa, ukisisitiza upendo, uaminifu, uvumilivu na heshima kati ya wanandoa.

Baadaye, aliendelea na kazi nyingine inayoitwa “Kaa Nami Bwana”, ambayo ujumbe wake unamwelekeza mwanadamu kumwomba Mungu awe karibu naye katika safari ya maisha.

Kupitia wimbo wake mpya wa “Nimemuona Bwana”, Jesca anaendelea kuonyesha dhamira yake ya kutumia kipaji cha muziki kama chombo cha kuhubiri Injili, kujenga imani na kuwafikishia watu ujumbe wa kumtambua na kumtegemea Mungu.

Wapenzi wa muziki wa Injili wanaweza kutazama video rasmi ya wimbo huo kupitia chaneli yake ya YouTube kwa kubofya kiungo hapa chini.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464