WANANCHI KIJIJI CHA ISELA WAMSHUKURU MBUNGE AZZA, ZAHANATI YAO YAFUNGULIWA NA KUANZA KUTOA HUDUMA
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
Wananchi wa Kijiji cha Isela Kata ya Samuye wilayani Shinyanga, wamemshukuru Mbunge wao wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad, kwa kutimiza ahadi yake juu ya ufunguzi wa Zahanati ya kijiji hicho, na kuanza kutoa huduma rasmi za matibabu.
TAZAMA VIDEO UFUNGUZI WA ZAHANATI👇👇
Hafla ya ufunguzi wa Zahanati hiyo imefanyika Oktoba 22,2026, na kuhudhuliwa na wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali na chama.
Mmoja wa wananchi hao Veronica Magaka, wamesema wanamshukuru Mbunge Azza kwa kutimiza ahadi yake juu ya ufunguzi wa Zahanati ya kijiji chao, na kuwasogezea huduma karibu na makazi yao, ambapo awali walikuwa wakiendea kupata huduma hiyo Kituo cha Afya Samuye.
Mwananchi mwingine Salome Yohana, amesema wanashukuru kuanza kutoa huduma za matibabu katika Zahanati yao na kuondokana na adha ya kufuata huduma za afya umbali mrefu.
Diwani wa Kata ya Samuye John Ngengeshi, amesema Zahanati ya Kijiji cha Isela ilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi tangu mwaka 2009 na imekamilika mwaka 2026 na kuanza kusuasua kufunguliwa, na kumshukuru Mbunge Azza kwa kutoa ahadi ya kufunguliwa kwa Zahanati hiyo na sasa imeanza kutoa huduma za matibabu.
Naye Mbunge wa Itwangi Azza Hillal Hamad, amesema Oktoba 1,2026 alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Isela kwa kusikiliza kero za wananchi, alipokea malalamiko juu kusuasua kufunguliwa kwa Zahanati ya kijiji hicho, ambapo alipiga simu kwa Mganga Mkuu wa Halmashauri kuuliza lini Zahanati hiyo itafunguliwa, na kupewa majibu kuwa itafunguliwa Oktoba 20 na sasa ameifungua na huduma zimeanza kutolewa.
Amesema, Oktoba 20 pia Zahanati ya Nshinshinuli iliyopo katika Jimbo hilo la Itwangi ilifunguliwa na Oktoba 22 Zahanati ya Isela nayo imefunguliwa na hivyo kufanya ndani ya miezi 9 ya Ubunge wake Zahanati mbili zimefunguliwa na kuanza kutoa za matibabu na hivyo kufikisha Zahanati 24 ambazo zinafanya kazi katika Jimbo hilo.
Amesema, hua ni mwanzo tu na safari ya miaka mitano ndiyo wameianza, na anatamani kuona Zahanati zote ambazo zilianzishwa kwa nguvu za wananchi zinakamilika na kuanza kutoa huduma, na nyingine amekuwa wakitoa fedha zake mfuko mfukoni kuzipauwa ili wananchi wapate huduma karibu na makazi yao.
Aidha, amesema katika Zahanati hiyo pia Mheshimiwa Rais Dk, Samia Suluhu Hassan, ameshatoa fedha sh. milioni 25 kwa ajili ya kununua vifaa kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma za uzazi ili kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Katika hatua nyingine ,amewataka wananchi kuwa na mahusiano ya karibu na watumishi wa afya katika Zahanati hiyo, huku akiwataka pia watumishi hao kutoa huduma bora za matibabu kwa wananchi.
Amewataka pia wananchi wa Kijiji hicho cha Isela, kujiunga pia na mfuko wa Bima ya afya kwa wote (NHIF) Sh. 150,000 kwa watu sita katika Kaya moja mwaka mzima, na kupata matibabu bure hadi kwenye hospitali kubwa za rufaa Bugando na Mhimbili.
TAZAMA PICHA👇👇
Mbunge wa Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza.
Mbunge wa Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza.
Mbunge wa Itwangi Azza Hillal Hamad akiangalia kuanza kwa utoaji wa huduma za matibabu katika Zahanati ya Isela mara baada ya kumaliza kuifunga.
Diwani wa Samuye John Ngengeshi akizungumza.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Damas Nyansila akizungumza.