` MBUNGE AZZA ATINGA ZAHANATI MPYA YA NSHISHINULU, ATATUA BAADHI YA CHANGAMOTO KWA VITENDO

WANDAMAN HOTEL

MBUNGE AZZA ATINGA ZAHANATI MPYA YA NSHISHINULU, ATATUA BAADHI YA CHANGAMOTO KWA VITENDO

 

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Mbunge wa Jimbo la Itwangi, Azza Hillal Hamad, ametembelea Zahanati mpya ya Kijiji cha Nshishinulu katika jimbo hilo na kutatua baadhi ya changamoto ambazo bado zinazoikabili, ikiwamo kuahidi kutoa kompyuta mpya ya kisasa aina ya HP pamoja na mizani ya kupimia uzito wa watoto wanapokwenda kliniki.

TAZAMA VIDEO👇👇



Ziara ya mbunge huyo imefanyika leo, Oktoba 24, 2026, akiwa ameambatana na Diwani wa Nsalala, Joseph Shoto, kwa lengo la kukagua utoaji wa huduma za matibabu katika zahanati hiyo tangu ilipofunguliwa rasmi Oktoba 20 mwaka huu.

Azza amesema, baada ya kufika katika zahanati hiyo na kuzungumza na Mganga Mfawidhi, ameelezwa mapungufu yaliyopo ambayo yanahitaji kutatuliwa, ili kuboresha huduma kwa wananchi.

Amesema, mojawapo ya changamoto kubwa ambayo ameelezwa na nihitaji la haraka, ni ukosefu wa kompyuta kwa ajili ya kutunza kumbukumbu za wagonjwa na kuwaandikia namba za malipo (Control Number), na ameahidi kutoa kompyuta hiyo leo.
“Changamoto ya ukosefu wa kompyuta nitaitatua leo leo, kwa sababu ni muhimu sana, pia nitanunua mizani ya kupimia uzito wa watoto wanapokuja kliniki,” amesema Azza.

Amesema, kwa changamoto nyingine zilizobaki, amezichukua na atakwenda kuikumbusha serikali ili izitatue na kuboresha huduma za afya katika zahanati hiyo.
Aidha, amewahimiza pia wananchi wa kijiji hicho kujiunga na mfuko wa bima ya afya kwa wote (NHIF), kwa kuchangia sh. 150,000 kwa mwaka, ambapo watu sita katika familia moja watanufaika na huduma za matibabu, zikiwamo zinazotolewa katika hospitali za rufaa pamoja na bugando.

Awali, Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo, Dk. Aman Kubuka, akiwasilisha baadhi ya changamoto kwa mbunge huyo, amesema kituo hicho kinakabiliwa na ukosefu wa umeme, hali inayosababisha jokofu la kuhifadhia chanjo kushindwa kufanya kazi.
Ametaja changamoto nyingine, ni ukosefu wa kompyuta, ambapo huduma za matibabu kwa sasa zinahitaji matumizi ya mifumo ya kielektroniki, ikiwamo kutengeneza namba za malipo (Control Number) kwa wagonjwa sababu kwa sasa hakuna malipo ya mkononi.

Changamoto zingine, amesema ni upungufu wa samani na vifaa muhimu, vikiwamo meza, viti, benchi za wagonjwa, makabati na rafu za kuhifadhia dawa.

Nao baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Nshishinulu, akiwamo Happynes Kaji, wamemshukuru Mbunge Azza kwa jitihada za kuwezesha zahanati hiyo kuanza kutoa huduma za matibabu, wakisema imewaondolea adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma katika kituo cha afya Tinde.

TAZAMA PICHA👇👇
Mbunge wa Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza na Mganga Mfawidhi Zahanati ya Kijiji cha Nshishinulu.
Mbunge wa Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nshishinulu.
Mbunge wa Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nshishinulu.
Mbunge wa Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nshishinulu.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464