` NAIBU WAZIRI WA MAJI ATEMBELEA MIRADI YA MAJI VISIMA JIMBO LA ITWANGI AMWAGIA SIFA MBUNGE AZZA KUWAPIGANIA WANANCHI WAKE

WANDAMAN HOTEL

NAIBU WAZIRI WA MAJI ATEMBELEA MIRADI YA MAJI VISIMA JIMBO LA ITWANGI AMWAGIA SIFA MBUNGE AZZA KUWAPIGANIA WANANCHI WAKE

NAIBU WAZIRI WA MAJI ATEMBELEA MIRADI YA MAJI VISIMA JIMBO LA ITWANGI AMWAGIA SIFA MBUNGE AZZA KUWAPIGANIA WANANCHI WAKE

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew, amefanya ziara katika jimbo la Itwangi kukagua miradi ya maji ya visima virefu, huku akimpongeza Mbunge wa Jimbo hilo Azza Hillal Hamad kwa kwakuwapigania wananchi wake katika kuhakikisha anawatatulia matatizo hayo.
TAZAMA VIDEO👇👇



Amebainisha hayo jana Oktoba 18,2026, wakati alipofanya ziara ya kutembelea mradi wa maji wa kisima kirefu katika shule ya Sekondari Kituli, pamoja na Visima vya Maji vilivyopo Kata ya Nsalala.
Amesema, Jimbo hilo la Itwangi limepata Mbunge Makini ambaye ni Mwakilishi wao mzuri, na amekuwa akijenga hoja mbele ya Bunge, Mawaziri, kwa kuwasemea matatizo wananchi wake jambo ambalo limekuwa likifanya serikali kutoa fedha na kuzileta Itwangi kutatua shida za wananchi.

“Ukiwa na Mbunge asiyeweza kujenga hoja na hoja isiyokuwa na tija na maslahi mapana ya wananchi hakuna Waziri utayemuona amefika kwenye Jimbo hilo,”Amesema Mhandisi Kundo.
Ameongeza kuwa, ukiona Mawaziri wanapisha katika Jimbo la Itwangi uelewa kwamba wananchi wa Itwangi mlifanya maamuzi sahihi, ya kumchagua Mbunge ambaye anajua maana ya uwakilishi wa wananchi.

Aidha, akizungumiza visima vya maji ambavyo amevitembelea kikiwamo cha shule ya Sekondari Kituli, ameagiza RUWASA kutoa kiasi cha fedha sh. milioni 100 kwa ajili ya kukikamilisha na kuanza kutoa huduma ya maji.
Amesema kuhusu visima vya Kata ya Nsalala, amesema visima hivyo vilikuwa vikipigiwa kelele na Mbunge Azza kila mara Mbunge, ambapo Rais Dk, Samia Suluhu Hassan, baada ya kusikilia kilio cha Mbunge dhidi ya wananchi wake atao maelekezo kwa Wizara ya Maji kufika Nsalala kwa ajili ya kuvikagua.

Amesema, baada ya Wizara kufika kwenye visima hivyo, wamejionea wenyewe kuwa vinauwezo mkubwa wa kuzisha maji ambapo kisima kimoja kinauwezo wa kutoa maji lita 12,000 kwa saa na kingine Lita 15,000 kwa saa, na kwamba visima hivyo haiwezi kushindwa kuhudumia wananchi wa vijiji vitatu vya Nsalala na wanakwenda kulifanyia kazi.
“Hapa tuna wataalamu wetu wa RUWASA na Bonde, maelekezo ni kwamba hiyo kazi hatutaki ichukue muda visima hivyo vikamilishwe kabla ya Januari 31,2027 na kuanza kutoa huduma kwa wananchi na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ameshatoa sh. milioni 100 fedha ambazo Azza aliziomba.” Amesema Mhandisi Kundo.

Aidha, amesema Wizara hiyo ya Maji, pia imeweka mipango ya kupeleka katika vijiji vyote nchini na kwamba nchi nzima kuna vijiji 12,333, na kati ya vijiji hivyo1,575 havina huduma ya maji, kwamba mkakati uliopo hadi kufika 2030 vijiji vyote vinapaswa viwe na huduma ya maji, na katika mwaka wa fedha 2026/2027 Wizara imeshatenga vijiji 400 kwa ajili ya kuvisambazia huduma hiyo, na program hiyo itakuwa ni mwendelezo kwa kila mwaka wa fedha kutenga vijiji 400.
Naye Mbunge wa Itwangi Azza Hillal Hamad, ameishukuru serikali chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kusikiliza kilio cha wananchi mara baada ya yeye kuwasemea Bungeni na kutoa fedha na kutatua shida za wananchi wa Itwangi.

Amesema, dhamira kuu ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ni kuhakikisha wanawake wanaondokana na shida ya kutafuta maji umbali mferu bali wafanye kazi na kukuza uchumi wao.

Amesema visima hivyo vya Maji, vinauwezo wa kuhudumia wananchi wa kijiji cha Welezo, Nsalala na Mwamkanga, na kuondokana kabisa na adha ya maji.

TAZAMA PICHA👇👇
Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew akizungumza na wananchi Nsalala Jimbo la Itwangi.
Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew akizungumza na wananchi Nsalala Jimbo la Itwangi.
Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew akizungumza na wananchi Nsalala Jimbo la Itwangi.
Mbunge wa Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza.
Mbunge wa Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza.
Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew (kulia) akikagua mradi wa maji wa visima virefu.









Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464