` NAIBU WAZIRI WA MAJI KUNDO MATHEW AKAGUA MRADI WA BILIONI 5.2 MSALALA, AWAHAKIKISHIA WANANCHI KUPATA HUDUMA YA MAJISAFI NA SALAMA

WANDAMAN HOTEL

NAIBU WAZIRI WA MAJI KUNDO MATHEW AKAGUA MRADI WA BILIONI 5.2 MSALALA, AWAHAKIKISHIA WANANCHI KUPATA HUDUMA YA MAJISAFI NA SALAMA




Na Marco Maduhu, KAHAMA

Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew, amewahakikishia wananchi wa Kata ya Jana Halmashauri ya Msalala, kuwa mradi wa upanuzi wa maji ambao unatekelezwa kwenye Kata hiyo, utakamilika na kutoa huduma ya majisafi na salama kwenye vijiji vyote vitano.

TAZAMA VIDEO👇👇


Amebainisha hayo leo Oktoba 18, 2026 wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya upanuzi wa mradi wa maji kutoka Kagongwa- Isaka kwenda vijiji vya Jana, Mwalugulu, Kilimbu, Butondolo, na Itongwang’holo.

Amesema, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ametoa maelekezo kwa Waziri wa Maji Jumaa Aweso, kufika Msalala kwenye mradi huo ambao umesua utekelezwaji wake, na kwamba kutokana na majukumu mengine aliyonayo yupo katika Ziara ya Makamu wa Rais. akamtuma yeye kupeleka ujumbe wa Rais Samia, kwamba mradi unakwenda kukamilika.
“Mradi huu ambao unaendelea hapa wa sh.bilioni 5 ambao mpaka sasa haujakamilika, Mheshimiwa Rais ametuelekeza kuja kutekeleza na kuhakikisha tunaleta fedha kiasi cha sh.milioni 490 katika Kata ya Jana ili kuukamilisha” amesema Mhandisi Kundo.

Aidha, amesema nchi nzima inajumla ya vijiji 12,333, na kati ya vijiji hivyo1,575 havina huduma ya maji, na kwamba mkakati uliopo hadi kufika 2030 vyote vitakuwa na huduma ya maji, na katika mwaka wa fedha 2026/2027, Wizara imetenga vijiji 400 kuvisambazia huduma hiyo, na ni mwendelezo wa kila mwaka wa fedha.
Katika hatua nyingine, ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuilinda miundombinu ya miradi ya maji, ili iweze kuwahudumia kwa muda mrefu.

Kwa upande wake Meneja wakala wa majisafi na usafi wa mazingira vijiji RUWASA wilaya ya Kahama Mhandisi Maduhu Magili, amesema utekelezwaji wa mradi huo ulianza 2022 na kwamba gharama zake ni bilioni 5.2 na sasa upo asilimia 68, na baadhi ya vijiji vitatu tayari vinatumia maji kasoro vijiji viwili na utanufaisha wananchi zaidi ya elfu 22, na unavituo vya kuchotea maji 31.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464