AZZA: JIMBO LA ITWANGI HATUNA SHIDA NA CHANZO CHA MAJI
Na Marco Maduhu, Stela Paul, SHINYANGA
Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad, amesema jimbo hilo halina shida na chanzo cha maji, sababu maji ya Ziwa Victoria tayari yapo.
TAZAMA VIDEO👇👇
Amebainisha hayo jana wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kazuni Kata ya Bukene kwenye mkutano wa hadhara wa kuwashukuru pamoja na kusikiliza kero zao na kuzipatia majibu.
Amesema, katika kijiji hicho cha Kazuni kuna mradi wa Maji ya Kisima kirefu, lakini maji hayo yana chumvi na wameshindwa kuyatumia.
“Kijiji chetu cha Kazuni ukisoma taarifa ya Wizara ya Maji kina onekana kina mradi wa maji ya kisima kirefu, lakini nimepata fursa ya kuongea na wananchi, wameniambia maji haya yanachumvi, uongo kweli,” amesema Azza.
Amesema ajenga ya maji ameibeba kama ya Jimbo, na kwamba katika vijiji 58 vya jimbo la Itwangi vijiji 9 vinasomeka vina maji ya kisima kirefu, na vijiji 14 vina maji ya Ziwa Victoria, na vijiji 34 havina maji kabisa.
Aidha, amesema katika jimbo hilo hawana shida na chanzo cha maji sababu maji ya Ziwa Victoria yapo jimboni humo na kuwatoa hofu wananchi wa kijiji hicho cha Kazuni kuwa maji hayo yapo karibu ambayo yatatolewa Bukeni na kuwafikia.
Katika hatua nyingine, amezungumzia uchakavu wa miundombinu ya vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Kazuni na kumpigia simu Afisa Mipango wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ili aweke mikakati ya maboresho ya shule hiyo.
Amewataka pia wananchi wa kijiji hicho cha Kazuni kuchukua tahadhari dhidi ya mvua za El-Nino hasa wale ambao wanaishi kwenye mabonde.
Changamoto nyingine zilizozungumzwa kwenye mkutano huo ni ukosefu wa mwalimu wa kike shule ya msingi Kazuni, nyumba ya walimu, ubovu wa miundombinu ya barabara, umeme kwa baadhi ya vitongoji na ukosefu wa Zahanati ya kijiji.
TAZAMA PICHA👇👇
Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kazuni.
Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kazuni.
Diwani wa Bukene Majaliwa Luhende akizungumza.































