` TAMASHA LA KIZIMKAZI NI NGUZO YA UMOJA, MSHIKAMANO NA UDUGU WA KITAIFA

WANDAMAN HOTEL

TAMASHA LA KIZIMKAZI NI NGUZO YA UMOJA, MSHIKAMANO NA UDUGU WA KITAIFA


Tamasha la Kizimkazi lililofanyika Zanzibar limetajwa kuwa jukwaa muhimu la kukuza umoja, mshikamano wa kitaifa, na udugu wa kudumu miongoni mwa Watanzania huku likiimarisha tunu ya Muungano .

Akizungumza kufuatia kufungwa kwa tamasha hilo, Mtaalam wa Maridhiano, Amani na Maendeleo, Dkt. Dennis Muchunguzi, aliwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za maendeleo ili kuchochea malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na kulinda amani ya nchi.

Aidha, aliongeza kuwa uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania Bara na Zanzibar una mizizi mirefu hata kabla ya Muungano, akitolea mfano wa mchezo wa soka kati ya timu za Simba na Yanga uliochezwa visiwani humo kama ushahidi wa mshikmano huo imara unaopaswa kulindwa kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Dkt. Muchunguzi amesisitiza kuwa mshikamano wa kitaifa ni msingi muhimu wa utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050, hususan katika juhudi za kuinua uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464