` SERIKALI YAENDELEA KUFIKISHA UMEME VIJIJINI, NDEJEMBI AWASHA UMEME MWANUBI - SHINYANGA

WANDAMAN HOTEL

SERIKALI YAENDELEA KUFIKISHA UMEME VIJIJINI, NDEJEMBI AWASHA UMEME MWANUBI - SHINYANGA

Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, akiweka mahindi kwenye mashine ya kusaga baada ya kuwasha rasmi umeme katika Kitongoji cha Mwanubi, mkoani Shinyanga, Agosti 10, 2026, akionesha namna nishati hiyo inavyoweza kutumika katika shughuli za uzalishaji na kuongeza kipato kwa wananchi. Picha na Elizabeth Cosmas - Malunde 1 blog
Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, akiweka mahindi kwenye mashine ya kusaga baada ya kuwasha rasmi umeme katika Kitongoji cha Mwanubi, mkoani Shinyanga, Agosti 10, 2026, akionesha namna nishati hiyo inavyoweza kutumika katika shughuli za uzalishaji na kuongeza kipato kwa wananchi.
Muonekano wa sehemu ya nyumba iliyofikishiwa huduma ya umeme katika Kitongoji cha Mwanubi kata ya Kolandoto, mkoani Shinyanga, Agosti 10, 2026, baada ya Serikali kupitia REA kuunganisha eneo hilo na huduma ya umeme. 

Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, akikata utepe kuashiria kuwashwa rasmi kwa umeme katika Kitongoji cha Mwanubi kata ya Kolandoto, mkoani Shinyanga, Agosti 10, 2026, ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali za kufikisha huduma ya umeme vijijini na vitongojini.
Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, akikata utepe kuashiria kuwashwa rasmi kwa umeme katika Kitongoji cha Mwanubi, mkoani Shinyanga, Agosti 10, 2026, ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali za kufikisha huduma ya umeme vijijini na vitongojini.

Na Elizabeth Cosmas – Malunde 1 Blog, Shinyanga

Jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, za kuhakikisha vijiji na vitongoji nchini vinafikishiwa huduma ya umeme zimeendelea kuzaa matokeo, baada ya Kitongoji cha Mwanubi mkoani Shinyanga kuunganishwa na huduma hiyo.

Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, amewasha rasmi umeme katika Kitongoji cha Mwanubi kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga leo, Agosti 10, 2026, akisema umeme ni hitaji la msingi kwa Watanzania na nyenzo muhimu katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Ndejembi amesema Serikali inaendelea kupanua miundombinu ya umeme vijijini na vitongojini ili kuwawezesha wananchi kutumia nishati hiyo katika shughuli za uzalishaji na kuboresha maisha yao.
Amesema kufikishwa kwa umeme kunapaswa kwenda sambamba na matumizi yenye tija, ikiwemo kuongeza thamani ya mazao, kukuza biashara, kuanzisha shughuli za uzalishaji na kuongeza kipato cha wananchi.

“Umeme siyo tu kwa ajili ya kuwasha taa, bali ni kichocheo cha uzalishaji na maendeleo. Wananchi wanapaswa kutumia fursa hii kuongeza thamani ya mazao, kukuza biashara na kuanzisha shughuli mbalimbali za kiuchumi,” amesema.

Ndejembi amewahimiza wananchi ambao miundombinu ya umeme imefika katika maeneo yao kuchangamkia fursa hiyo kwa kuunganishiwa huduma kwa gharama ya Shilingi 27,000 na kuitumia katika shughuli zitakazowaongezea kipato.

Aidha, ameiagiza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kufanya tathmini ya maeneo ambayo bado hayajafikiwa na miundombinu ya umeme ili yaingizwe katika mipango ya utekelezaji na kufikishiwa huduma hiyo.
Pia amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme kuongeza kasi ya usimikaji wa nguzo na ujenzi wa miundombinu katika maeneo yaliyosalia ili wananchi wengi zaidi waweze kufikiwa na kuunganishiwa huduma.

Amesisitiza kuwa shule, zahanati na maeneo mengine ya huduma za kijamii yanapaswa kupewa kipaumbele katika kufikishiwa umeme kutokana na umuhimu wake katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Ndejembi amesema Serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kutekeleza miradi ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa nishati ya uhakika na kufungua fursa za kiuchumi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, ameishukuru Serikali kupitia REA kwa kufikisha huduma ya umeme katika vijiji vyote vya Mkoa wa Shinyanga, akisema hatua hiyo imefungua fursa mpya za maendeleo kwa wananchi.

Mhita amesema upatikanaji wa umeme vijijini umechangia kuboresha shughuli za kiuchumi, uzalishaji, ajira na huduma za kijamii, huku akieleza kuwa hatua inayofuata ni kuhakikisha vitongoji vilivyosalia vinafikiwa na huduma hiyo.

Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mha. Herini Mhina, amesema Wakala unaendelea kutekeleza miradi ya kusambaza umeme katika vitongoji mbalimbali nchini ili kuhakikisha wananchi wengi zaidi, hususan walioko maeneo ya vijijini, wanapata huduma hiyo.
Amesema REA itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi hiyo ili kupanua wigo wa upatikanaji wa umeme na kuwawezesha wananchi kutumia nishati hiyo katika shughuli za kiuchumi, uzalishaji na utoaji wa huduma za kijamii.

Diwani wa Kata ya Kolandoto, Mshagatila Moses, amesema anawashukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwafikishia wananchi wa Kitongoji cha Mwanubi huduma ya umeme, akieleza kuwa nishati hiyo itachochea shughuli za kiuchumi na kuboresha maisha ya wananchi.

Wananchi wa Kitongoji cha Mwanubi wameishukuru Serikali kwa kuwafikishia huduma ya umeme, wakisema hatua hiyo itafungua fursa mpya za biashara na uzalishaji pamoja na kuongeza thamani ya mazao.

Wamesema upatikanaji wa umeme utawasaidia kuanzisha na kuendeleza shughuli mbalimbali za kiuchumi, huku ukiboresha mazingira ya utoaji wa huduma muhimu za kijamii katika eneo hilo.
Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Mwanubi, mkoani Shinyanga, Agosti 10, 2026, wakati wa hafla ya kuwasha rasmi umeme katika eneo hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Mwanubi, mkoani Shinyanga, Agosti 10, 2026, wakati wa hafla ya kuwasha rasmi umeme katika eneo hilo.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mha. Herini Mhina, akitoa taarifa kwa wananchi wa Kitongoji cha Mwanubi, mkoani Shinyanga, Agosti 10, 2026, kuhusu utekelezaji wa miradi ya umeme na upanuzi wa huduma hiyo katika maeneo ya vijijini na vitongojini.

Diwani wa Kata ya Kolandoto, Mshagatila Moses, akizungumza wakati wa hafla ya kuwasha umeme katika Kitongoji cha Mwanubi, mkoani Shinyanga.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464