AZZA AWAHAKIKISHIA WANANCHI MAENDELEO MAKUBWA ITWANGI, AKISIKILIZA KERO ZA WANANCHI WA NG’WANHALANGA
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad, amesema ndani ya miezi sita baada ya kuapishwa pamoja na Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inasema kuanzia 2025 hadi 2030 vitongoji vyote vitakuwa na umeme.
TAZAMA VIDEO👇👇
Amebainisha hayo jana, wakati akisikiliza kero za wananchi wa Kijiji cha Ng’wanhalanga Kata ya Samuye wilayani Shinyanga.
Amesema, ndani ya miezi hiyo sita Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, ameshapeleka umeme katika Kitongoji cha Manonga na nguzo tayari zimeshafika.
Aidha, amesema pia Rais Dk. Samia ametengeneza barabara ya kuunganisha na wilaya ya Igunga kupitia mto manonga.
Ameongeza kuwa, katika kipindi cha kampeni, alipewa changamoto katika shule ya msingi Manongo, na kwamba ndani ya miezi hiyo sita zimepelekwa sh.milioni 25 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili.
“Ndani ya miezi sita tumeshuhudia maendeleo makubwa katika kijiji hiki cha Ng’wanhalanga, tunamshukuru sana Rais wetu Dk. Samia Suluhu Hassan,” amesema Azza.
Aidha, amesema jimbo hilo la Itwangi ndani ya miaka mitano kutakuwa na maendeleo makubwa.
Nao baadhi wa wananchi wa kijiji hicho waliwasilisha kero zao mbalimbali zikiwamo ya umeme, miundombinu ya barabara pamoja na maji.
TAZAMA PICHA👇👇
Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza.
Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akisikiliza kero za wananchi.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Itwangi Said Nasorro akizungumza.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464