TAZAMA VIDEO-MBUNGE AZZA AKABIDHI GARI LA WAGONJWA KITUO CHA AFYA TINDE
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad, amekabidhi gari la kubeba wagonjwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Dk. Kalekwa Kasanga, kwa ajili ya kuanza kutoa huduma katika Kituo cha Afya Tinde, hatua inayolenga kutatua changamoto ya usafiri wa dharura na kuokoa afya za wananchi.
TAZAMA VIDEO 👇👇
Akikabidhi gari hilo leo Julai 18, 2026, na kueleza kuwa anazitambua vyema shida za wananchi wa jimbo lake la Itwangi, ikiwamo ukosefu wa gari la wagonjwa katika kituo hicho cha afya, jambo lililomsukuma kupambana na kutafuta gari hilo ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji rufaa au huduma za dharura.
"Niliwaambia matatizo ya wananchi wa Tinde na Jimbo la Itwangi kwa ujumla nayafahamu, najua majukumu yangu. Kuwatekelezea maendeleo wananchi si lazima uwe na fedha mfukoni, bali uwe na uwezo wa kusimama na kubeba matatizo yao," amesema Azza.
Amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kupeleka miradi ya maendeleo katika Jimbo la Itwangi, akisema Serikali imeonyesha dhamira ya dhati ya kuboresha huduma mbalimbali kwa wananchi zikiwamo za afya.
Naye Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Tinde Evansi Munisi, amesema kuwa gari hilo litakuwa msaada mkubwa katika kuokoa afya za wananchi, hususan katika kuwakimbiza wagonjwa kwa haraka kwenda kupata matibabu zaidi kwenye hospitali za rufaa.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Dk. Kalekwa Kasanga, amesema huduma ya afya ni muhimu na kumshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha huduma za afya nchini huku akimshukuru pia Mbunge Azza kwa juhudi zake za kufanikisha kupatika kwa gari hilo la wagonjwa, na kuahidi kulitunza na kusimamia matumizi sahihi.
Mmoja wa wananchi wa Tinde Prisca Misaka, amebainisha kuwa gari hilo litakuwa mkombozi mkubwa kwao, hasa pale wanapokabiliwa na dharura za matibabu.
TAZAMA PICHA👇👇
Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza.
Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Edward Ngelela akizungumza.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Seth Msangwa akizungumza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Dk.Kalekwa Kasanga akizungumza.
Mganga Mfawidhi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Dk. Nuru Yunge akizungumza.
Naye Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Tinde Evansi Munisi,akiwasilisha taarifa.
Mbunge wa Itwangi Azza Hillal Hamad (kushoto) akikata utepe kumkabidhi gari la kubeba wagonjwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Dk. Kalekwa Kasanga (kulia) kwa ajili ya kituo cha afya Tinde.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464