TAZAMA VIDEO-MAHAFALI YA KWANZA YA SENETI MKOA WA SHINYANGA YAFANYIKA
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
Mahafali ya kwanza ya Seneti ya wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo vya kati Mkoa wa Shinyanga yamefanyika kwa mafanikio makubwa, huku Rais Dk. Samia Suluhu Hassan akipongezwa kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya elimu ya juu uliowezesha vijana wengi kupata fursa ya kujiunga na vyuo na kutimiza ndoto zao.
TAZAMA VIDEO👇👇
Mahafali hayo yamefanyika leo, Julai 12, 2026, katika Ukumbi wa Mikutano wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha kundi la vyuo vikuu na vyuo vya kati, Dk. Regina Malima.
Akizungumza na wahitimu hao, Dk. Malima alisema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imefanya uwekezaji mkubwa katika vyuo vya kati, ikiwemo Mkoa wa Shinyanga, hatua iliyowezesha vijana wengi kupata nafasi ya kujiunga na vyuo hivyo.
Amesema, serikali pia imetatua changamoto ya upatikanaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, ambapo mikopo hiyo kwa sasa imekuwa ikitolewa kwa wakati, na zaidi ya Sh. bilioni 900 zimewekezwa katika mpango huo..
"Rais Samia ametatua changamoto ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo, mikopo hiyo sasa inatolewa kwa wakati, na hata wanafunzi wa vyuo vya kati wanaosomea Diploma nao wanapata mikopo," amesema Dk. Malima.
Aidha, amewataka vijana hao wanapohitimu masomo yao wasikae mitaani, bali wajifunze mbinu mbalimbali na kutumia vipaji vya kujiajiri, sababu mitaji yao wanayomikononi.
Amewasihi pia watumie Tekinolojia vizuri kwa manufaa na siyo kuitumia vibaya, na kwamba watu wengi wamepata ajira kupitia mitandao ya kijamii.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Katibu wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Naibu Katalambula, amesema mahafali hayo yamefanyika kwa mara ya kwanza kutokana na ongezeko la vyuo mkoani humo, lililotokana na uwekezaji uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita.
Pia, amewataka vijana kuendelea kudumisha amani na utulivu wa nchi, akisisitiza kuwa bila amani hakuna maendeleo, wala sehemu nyingine ya kukimbilia.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Seneti Mkoa wa Shinyanga Jackson Mwizarubi, amesema lengo la Seneti ni kuhakikisha wanafunzi wa vyuo wanajenga imani kwa serikali yao na viongozi waliopo madarakani.
Aidha, ameishukuu serikali kwa kuanza kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya kati, huku akiomba huduma za bima ya afya zijumuishwe katika mikopo hiyo, ili wanafunzi wanapougua waweze kupata matibabu bila changamoto.
Katika hatua nyingine, ameomba semina zaidi zitolewe kwa vijana ili kuwajengea uwezo wa kutambua na kutumia fursa mbalimbali za kiuchumi, akisema kuwa kuna maisha mara baada ya kumaliza chuo.
TAZAMA PICHA👇👇
Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha kundi la vyuo vikuu na vyuo vya kati, Dk. Regina Malima akizungumza.
Mwenyekiti wa SENETI Mkoa wa Shinyanga Jackson Mwizarubi akizungumza.
Katibu wa SENETI Mkoa wa Shinyanga Lukomanga Jinyange akizungumza.
Katibu wa Hamasa na Chipukizi Mkoa wa Shinyanga Anorld Rweichum akizungumza.
Peter Frank (Mr. Black) akizungumza.
Keki ya Mafahali ya SENETI.
Mgeni Rasmi akimlisha Keki Mwenyekiti wa Seneti Mkoa wa Shinyanga.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464