` ALLY HAPI AWATAKA VIONGOZI WA CCM KUSHUGHULIKIA MATATIZO YA WANANCHI

WANDAMAN HOTEL

ALLY HAPI AWATAKA VIONGOZI WA CCM KUSHUGHULIKIA MATATIZO YA WANANCHI

 

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Taifa Ally Hapi, amewataka wana CCM Mkoani Shinyanga, wasibweteke na ushindi ambao wameupata kwenye uchaguzi mkuu uliopita Oktoba 29 mwaka jana, bali washughulike na matatizo ya wananchi, kwa kutatua kero zao mbalimbali.

TAZAMA VIDEO👇👇

Amebainisha hayo leo Juni 4,2026 wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa CCM Mkoani Shinyanga kwenye ziara yake ya kuimarisha Chama mkoani humo, pamoja na kuendelea kujenga uhusiano mzuri kati ya CCM na wananchi.

Amesema, huko mbele kuna kazi kubwa zaidi, bali viongozi wa CCM wanapaswa kufanya kazi yao ya Chama, kwa kushughulika na matizo ya wananchi, na siyo kutegemea serikali iwafanyie kazi zao.

“Chama kikisikia wafanyabiashara wanataharuki lazima wawe wakwanza kwenda eneo la tukio kusikiliza matatizo yao, sababu wao ndiyo wenye dhamana ya serikali ambayo ipo madarakani, na kutoa maelekezo ya utatuzi wa kero zao,” amesema Hapi.

 

Aidha, amewataka pia viongozi wanaotokana na dola wakiwamo Wabunge, Madiwani, Wenyeviti wa Mitaa na vijji, kuhakikisha wanatembelea maeneo yao mara kwa mara, kwa kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo, na kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.

Katika hatua nyingine amewataka wazazi kuwalea watoto wao katika maadili mema, pamoja na kusimamia maadili ya vijana, ikiwamo kuwafundisha madarasa ya itikadi.

TAZAMA PICHA👇👇

Katibu wa Jumuiya wa wazazi CCM Taifa Ally Hapi akizungumza.

Katibu wa Jumuiya wa wazazi CCM Taifa Ally Hapi akizungumza.
Katibu wa Jumuiya wa wazazi CCM Taifa Ally Hapi akizungumza.
Katibu wa Jumuiya wa wazazi CCM Taifa Ally Hapi akizungumza.
Katibu wa Juiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga Rejina Ndulu.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo akizungumza.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akizungumza.
Katibu wa Jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Dorisi Kibabi (kushoto), akiwa na Katibu wa Jumiya ya wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga Rejina Ndulu kwenye mkutano.
Katibu wa Jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Dorisi Kibabi (kushoto), akiwa na Katibu wa Jumiya ya wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga Rejina Ndulu kwenye mkutano.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464