` MANISPAA YA SHINYANGA KUENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI

WANDAMAN HOTEL

MANISPAA YA SHINYANGA KUENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI

Manispaa ya Shinyanga kuendelea kutatua changamoto za wananchi

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MEYA wa Manispaa ya Shinyanga, Salum Kitumbo, amewataka madiwani kuendelea kushirikiana na wataalamu katika kusimamia miradi ya maendeleo, na kuwahudumia wananchi katika kutatu changamoto zinazowakabili.
Amebainisha hayo leo Mei 8, 2026 wakati akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani cha Manispaa hiyo.


Amesema, wananchi wanawategemea viongozi wao katika kuwahudumia na kuwaletea maendeleo, hivyo ni muhimu Madiwani na Walaamu kufanya kazi kwa ushirikiano na kwa moyo wa dhati.
“Wananchi wanatutegemea sana sisi, hivyo tuwe wa moja madiwani na watumishi katika kuleta tabasamu kwa wananchi wetu,” amesema Kitumbo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze, amesema yote yaliyojadiliwa kwenye kikao hicho yatafanyiwa kazi, huku akiahidi kuendelea kushirikiana na madiwani katika kusukuma gurudumu la maendeleo la manispaa hiyo.

Katika kikao hicho cha baraza, yalijadiliwa pia masuala mbalimbali yakiwamo ya masoko, elimu na miundombinu ya barabara.

TAZAMA VIDEO CHINI YA PICHA👇👇
Meya wa Manispaa ya Shinayanga Salum Kitumbo akizungumza kwenye Baraza la Madiwani.
Meya wa Manispaa ya Shinayanga Salum Kitumbo akizungumza kwenye Baraza la Madiwani.
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Pendo Sawa akizungumza kwenye Baraza.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze akizungumza kwenye Baraza.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Anorld Makombe akizungumza kwenye Baraza.
VIDEO KWA CHINI

t

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464