` KANISA LA SAYUNI LATOA MSAADA KWA WAHITAJI

WANDAMAN HOTEL

KANISA LA SAYUNI LATOA MSAADA KWA WAHITAJI

 


Kanisa la Sayuni latoa msaada kwa watu wenye uhitaji

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Kanisa la Sayuni lililopo Kata ya Mwawaza Manispaa ya Shinyanga, limefanya matendo ya huruma kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali kikiwamo chakula kwa watu wenye uhitaji.

TAZAMA VIDEO👇👇
Msaada huo umetolewa leo Mei 31,2026 Kanisani hapo.

Mwangalizi wa Kanisa hilo Anold Makombe, amesema wameona ni vyema kufanya matendo ya huruma, kwa baadhi ya washiriki na jamii ambayo inawazunguka ambao wanauhitaji kwa kutoa chakula, ikiwamo unga,mafuta ya kula,sukari ,mafuta ya kujipaka, viberiti, chumvi na sabuni.
Diwani wa Mwawaza Edwin Washa, ameshukuru Kanisa hilo kwa kuguswa na watu wenye uhitaji, na kuwapatia misaada mbalimbali ikiwamo chakula.

Nao baadhi ya wahitaji hao akiwamo Mariam Bundala, wamesema wanashukuru kwa msaada huo wa chakula, na kuwaombea waliojitoa kwamba Mungu awabariki na waendelee na moyo huo huo wa kujitoa.

MAELEZO KATIKA PICHA👇👇
Mwangalizi wa Kanisa la Sayuni Kata ya Mwawaza Anold Makombe akizungumza.
Diwani wa Mwawaza Edwin Washa akizungumza.
Msaada wa chakula ukitolewa kwa wahitaji.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464