` JESCA SIMUCHILE FT EV. DANIEL SAFARI WAACHIA VIDEO MPYA YA INJILI “TUIMBE TUMEPONA”

WANDAMAN HOTEL

JESCA SIMUCHILE FT EV. DANIEL SAFARI WAACHIA VIDEO MPYA YA INJILI “TUIMBE TUMEPONA”

 




Muimbaji wa muziki wa injili Jesca Simuchile kwa kushirikiana na Ev. Daniel Safari wameachia rasmi video mpya ya wimbo wao unaoitwa “Tuimbe Tumepona”, kazi yenye ujumbe wa matumaini, ushuhuda na kumshukuru Mungu kwa wema wake.

 Kupitia sauti zao zenye mguso wa kiroho pamoja na mpangilio mzuri wa video ya kiwango cha 4K, Jesca Simuchile na Ev. Daniel Safari wameonesha ubunifu mkubwa katika kazi hiyo mpya ya injili.

Kupitia kazi hiyo, Jesca Simuchile anaendelea kuthibitisha uwezo wake mkubwa katika muziki wa injili kutoka mkoani Shinyanga huku mashabiki wake wakitarajia kuona kazi nyingine nyingi zaidi kutoka kwake katika kipindi hiki cha huduma na muziki.

Tazama Video hapa chini
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464