` MADIWANI WAKUMBUSHWA WAJIBU WA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

WANDAMAN HOTEL

MADIWANI WAKUMBUSHWA WAJIBU WA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

 

MADIWANI WAKUMBUSHWA WAJIBU WA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MADIWANI wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wamekumbushwa kufanya mikutano ya hadhara kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Wito huo umetolewa leo Mei 6,2026 na Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Omary Mwenda, wakati akitoa salama za Mkuu wa wilaya hiyo Julius Mtatiro kwa niaba yake kwenye kikao cha baraza la madiwani.
Amesema, madiwani wanadhamana ya kusikiliza kero na malalamiko ya wananchi kwa ngazi zao, na kuzitafutia majibu ambazo zipo ndani ya uwezo wao, ili kuwapunguzia pia mzigo wananchi wa kutembea umbali mrefu kwenda kwenye Ofisi ya Mkuu wa wilaya kuwasilisha changamoto zao.

“Waheshimiwa madiwani nawakumbusha suala la kushughulikia kero za wananchi kwa kufanya mikutano mbalimbali, kama ambavyo amekuwa wakifanya Mkuu wa wilaya, sababu na nyie mnadhamana ya kufanya mikutano hiyo na kutatua migogoro ya wananchi ambayo ipo ndani ya uwezo wenu,”amesema Mwenda.
Amewasisitiza pia wataalamu wa halmashauri, kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na madiwani ikiwamo kusimamia shughuli za serikali pamoja na miradi ya maendeleo.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Seth Msangwa, amesema nasaha zote ambazo zimetolewa na viongozi kwenye baraza hilo, watazisimamia na kuzitekeleza, kwa mustakabali wa wananchi wa halmashauri hiyo

TAZAMA PICHA👇👇
Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Omary Mwenda, akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Edward Ngelela akizungumza.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Seth Msangwa akizungumza.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464