` BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA LAPOKEA TAARIFA ZA MAENDELEO YA KATA

WANDAMAN HOTEL

BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA LAPOKEA TAARIFA ZA MAENDELEO YA KATA

 




Na Marco Maduhu, SHINYANGA

BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga limekutana leo Mei 5, 2025 na kupokea taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo kutoka kwa madiwani katika kata zao, likilenga kutathmini maendeleo na changamoto zinazokabili maeneo yao.

Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo, kiliwakutanisha madiwani, watendaji pamoja na wakuu wa idara, ambapo kila diwani aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli katika kata yake.
Akiwasilisha taarifa ya Kata ya Mwakitolyo, Diwani Masalu Nyese alisema bado wanakabiliwa na changamoto ya mgogoro wa tozo kubwa kwa wachimbaji madini, hali inayodaiwa kusababisha kusimama kwa shughuli za uzalishaji na kuikosesha mapato halmashauri.

“Kwenye kata yangu bado kuna changamoto ya utatuzi wa mgogoro wa tozo kwa wachimbaji, ambao umesababisha shughuli za uzalishaji kukwama. Tunaomba suluhu ya haraka ili shughuli ziendelee na halmashauri ipate mapato,” amesema Nyese.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Seth Msangwa, alisema tayari wameunda tume kushughulikia suala hilo na kwamba wanasubiri majibu yake, huku akikiri kuwa changamoto hiyo imeathiri ukusanyaji wa mapato ya halmashauri.

TAZAMA PICHA👇👇
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Seth Msangwa akizungumza kwenye kikao cha baraza .
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Joseph Ntomela akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464