` WAUMINI WA DINI YA KIKRISTO WAASWA KUIFANYA PASAKA HII KUWA MWANZO MPYA WA MAISHA YAO

WANDAMAN HOTEL

WAUMINI WA DINI YA KIKRISTO WAASWA KUIFANYA PASAKA HII KUWA MWANZO MPYA WA MAISHA YAO


      Na Mwandishi wetu kutika  Mkoani Shinyanga......

Askofu wa kanisa la KKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victiria Dkt. Yohana Ernest Nzelu amewataka waumini wa Dini ya Kikristo kuifanya pasaka hii iwe mwanzo mpya wa maisha ya kumcha Mwenyezi Mungu, kuimarisha matumaini, upendo na mshikamano ili kuishi maisha yanayompendeza Mungu wakati huu wa maisha yenye misukosuko ya kila aina yanayoweza kupotosha imani za waamini wa Yesu Kristo.

Askofu Dkt. Nzelu ameyasema wakati akihubiri kwenye ibada ya Pasaka leo tarehe 5 April. 2026 katika kanisa kuu la KKT Ebenezer mjini Shinyanga.

Aidha Askifu Dkt Yohana Ernrst Nzelu amezungumza na wazazi na walezi akiwasihi kuimarisha malezi mema kwa watoto na familia zao huku wakikumbuka kuwaungamanisha na neno la Kristo Yesu kama ushuhuda wa wokovu wa mwanadamu.

Akizungumzia maisha ya ulimwengu wa sasa, Dkt. Nzelu amesema kumekuwa na changamoto ya masikio ya wanadamu kudaka zaidi matukio ya udaku hali inayoendelea kusababisha kuporomoka kwa maadili.

Hata hivyo amesema muarobaini wa hayo ni kumcha Mwenyezi Mungu na kutotishwa na kelel za dunia sambamba na kuntegemea Mungu kupitia ufufuko wa Bwana Yesu Kristo.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464