Mkurugenzi wa taasisi ya Joseph Muhunda Nyerere Foundation akipanda mti katika hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga
Stella Herman,Shinyanga
Taasisi ya Joseph Muhunda Nyerere Foundation imeadhimisha miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa vitendo kupitia zoezi la upandaji miti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na kuenzi umoja wa kitaifa.
Kupitia zoezi hilo, taasisi imeonesha dhamira yake ya kuunganisha maadhimisho ya kitaifa na shughuli za maendeleo zinazogusa maisha ya wananchi, hususan katika sekta ya afya na mazingira.
Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Joseph Muhunda Nyerere, amesema kuwa ni muhimu kwa jamii kuadhimisha Muungano kwa kufanya matendo yenye tija, ikiwemo kulinda mazingira kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Ameeleza kuwa upandaji miti una mchango mkubwa katika kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuboresha hali ya hewa, jambo linalochangia ustawi wa afya za wananchi.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Manispaa ya Shinyanga, aliyeshuhudia historia ya Muungano, alikumbusha kuwa alipata Muungano akiwa na umri wa takribani miaka 10, akisisitiza kuwa amani iliyojengwa tangu wakati huo imeendelea kuwa msingi imara wa kudumisha umoja na maendeleo ya Taifa.
Kwa ujumla, Taasisi ya Joseph Muhunda Nyerere Foundation imeendelea kuonesha mfano kwa kushiriki shughuli za kijamii na kuhamasisha utunzaji wa mazingira, ambapo upandaji miti umebaki kuwa miongoni mwa vipaumbele vyake katika kujenga jamii bora na endelevu.

Kwa upande wake, Mratibu wa Taasisi hiyo katika Manispaa ya Shinyanga, Mwalimu Leonard Mapolu, amesema wamekuwa wakitekeleza kampeni mbalimbali za mazingira na wataendelea kushirikiana na wadau kuhakikisha mji wa Shinyanga unakuwa wa kijani na salama kiafya.
Akizungumza kwa niaba ya hospitali, Mganga Mfawidhi Dkt. Luzila John ameishukuru taasisi hiyo kwa kuchagua eneo hilo, akieleza kuwa miti iliyopandwa itasaidia kuboresha mazingira ya hospitali na kuongeza upatikanaji wa hewa safi kwa wagonjwa na watumishi wa afya.