
Mwenyekiti wa Tume ya uchunguzi wa vurugu za wakati wa uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 Mhe. Jaji Mohamed Chande anairejesha jamii ambayo inaaminishwa kuwa Kila anayepotea anakuwa kapotezwa.
Akitoa ufafanuzi Aprili 28,2026 mbele ya waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Jaji Chande alifafanua kuwa ni vema jamii ikajua tofauti ya maneno kupote na kupotezwa.
Alisema kupotea ni mtu kutojulikana na ndugu na jamaa zake aliko ambapo anaweza kupotea kwa hiari yake au kupotea bila hiari yake.
Aidha alisema kupotezwa maana yake ni kukamatwa na kunyimwa Uhuru wake.
Katika ufafanuzi huo wa Jaji Chande kunaibua Mwanga mpana kwa jamii kuelewa kuwa si kila mtu anayepotea anakuwa kapotezwa, hivyo ni vema kila mmoja wetu akawa na utulivu wa kufikiri badala ya kuambukizwa fikra zisizo sahihi ambazo zinakuwa na malengo mapana ya siasa na kuikosanisha Serikali na wananchi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464