` KAHAMA KUVUNJA MBAVU MKESHA WA PASAKA NA COMEDY SHOW KUTOKA LAKE TALENT

WANDAMAN HOTEL

KAHAMA KUVUNJA MBAVU MKESHA WA PASAKA NA COMEDY SHOW KUTOKA LAKE TALENT

KAHAMA KUVUNJA MBAVU MKESHA WA PASAKA NA COMEDY SHOW KUTOKA LAKE TALENT

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

WAKAZI wa Kahama mkoani Shinyanga, wanatarajiwa kupata burudani ya vichekesho Jumamosi ya Mkesha wa Pasaka kupitia tamasha la ‘Live Comedy Show’ lililoandaliwa na Lake Talent kwa kushirikiana na Jambo Media.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 3,2026, Meneja wa Vipindi na Ubunifu wa Jambo Media Renatus Kiluvia maarufu ‘Bizzo Fresh’, amesema maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika na litafanyika katika ukumbi wa Malex Hall hapo Kesho.

Amesema, tamasha hilo linalenga kutoa burudani kwa wananchi pamoja na kukuza vipaji vya vijana katika tasnia ya vichekesho.
“Stand-up comedy imekuwa chanzo cha ajira kwa vijana wengi, na sasa imebadilika kutoka uchekeshaji wa kawaida hadi kuwa biashara inayowaingizia kipato. sisi kama Jambo Media tumeamua kuwaunga mkono vijana hawa,” amesema Kiluvia.

Amewataja, wachekeshaji watakaotumbuiza siku hiyo kuwa ni Wanani, Dogo Pepe, MC Ndembo, Shaf Brand, Godfrey Steven, Man Kush kutoka Kenya, MC Ndabitha, Miss Daines na Jo Master.
Kuhusu viingilio, amesema tiketi za Platinum ni Sh.15,000 kwa ununuzi wa mtandao, na Sh,20,000 mlangoni, huku Gold VIP Royal Sofa ni Sh150,000 kwa mtu mmoja na Sh,250,000 kwa watu wawili.

Amesema tiketi hizo zinapatikana katika maeneo mbalimbali ikiwemo Vunja Bei, Magic 101, Best Choice Store, Sodox Fashion, JJ Cosmetic na Kichomi Studio, na kwamba mtu atakaye hitaji kupata huduma ya kupelekewa tiketi apige simu namba 0754-418189 na 0787-581013.
Kwa upande wake, kiongozi wa kundi la wachekeshaji hao, Jo Master, amewataka wakazi wa Kahama kujitokeza kwa wingi kushuhudia tamasha hilo, akiahidi burudani ya hali ya juu.

Amesema tamasha hilo litakuwa la kipekee, na wamejipanga kuhakikisha wanawapa burudani itakayowafanya kuvunja mbavu.

MAELEKEZO KATIKA PICHA👇👇
Meneja wa Vipindi na Ubunifu wa Jambo Media Renatus Kiluvia maarufu ‘Bizzo Fresh akizungumza na waandishi wa habari.

Jo Master akizungumza na waandishi wa habari.
Jo Master akizungumza na waandishi wa habari.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464