Picha ya pamoja ya wadhamini na viongozi wa AIESEC Tanzania
Wanafunzi na wageni waalikwa wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa kongamano la AIESEC lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro

Wafanyakazi wa Barrick katika kongamano hilo
***
Wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani Morogoro wamepata fursa ya kupata elimu ya kuchangamkia fursa za kupata mafanikio kupitia elimu yao katika kongamano lililoandaliwa na taasisi ya AIESEC lililodhaminiwa na Barrick kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Katika kongamano hilo la aina yake, lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Mzumbe wanafunzi wameweza kujua kwa undani shughuli za makampuni mbalimbali makubwa ya kibiashara nchini na jinsi ya kutafuta fursa ya kujiunga nayo pindi wamalizapo masomo yao ya elimu ya juu.
Wanafunzi pia wamejengewa uwezo kutoka kwa wafanyakazi wa Barrick nchini na taasisi nyinginezo kuhusiana na jinsi ya kuchangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza,kujiamini na jinsi ya kujiajiiri na kutengeneza fursa za ajira.
Barrick Tanzania yenye ubia na Serikali kupitia kampuni ya Twiga imekuwa na programu mbalimbali za kuwezesha na kuinua vipaji vya vijana wa kitanzania wakiwemo wanafunzi wanaosoma katika vyuo mbalimbali na inayo programu maalumu ya kujenga kizazi kijacho cha wataalamu wa sekta ya madini ambayo tayari imeanza kutekelezwa.












