.jpg)
Wakati vizabizabina wakihangaika mitaani kupiga kelele zisizo na tija, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya usukani wa shupavu Dkt. Samia Suluhu Hassan, inaendelea kuandika historia mpya kwa kuishangaza dunia.
Safari hii, salamu zimetoka jijini Washington, Marekani, ambapo Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amezizima "Powering Africa Summit" kwa kunadi utajiri wa kutisha wa futi trilioni 57.54 za gesi asilia ambazo sasa zinaifanya Tanzania kuwa lulu ya uwekezaji barani Afrika.
Kwa wale wasioelewa, amani na utulivu uliopo nchini chini ya uongozi wa Mama Samia ndio "viza" pekee inayowezesha rasilimali hizi kuanza kuchimbwa na kuwanufaisha wananchi.
Bila amani, gesi hiyo ingebaki ardhini, lakini kwa utulivu huu, Tanzania sasa inaingia kwenye hatua ya kugeuza uchumi wa taifa kuwa wa kisasa zaidi kuelekea Dira ya 2050. Hii ni dhihaka tosha kwa wanaodai kuwa hakuna kinachofanyika—Mama anapiga kazi, na matokeo yanaonekana hadi Marekani!
Waziri Makamba ameweka wazi kuwa licha ya utajiri huo uliothibitishwa, takribani asilimia 70 ya maeneo yenye uwezekano wa kuwa na mafuta na gesi bado hayajaguswa. Hii ni fursa adhimu kwa wawekezaji wakubwa duniani kuingia nchini kuanza utafutaji na uchimbaji. Serikali iko mbioni kutoa vitalu vipya vya utafutaji na kutekeleza mradi mkubwa wa kuchakata gesi kuwa kimiminika (LNG), mradi utakaofungua masoko ya dunia na kumwaga mabilioni ya fedha kwenye pato la taifa.
Serikali ya Awamu ya Sita haina maneno mengi, bali ina vitendo vya mfano. Lengo ni kuona gesi hii inatumika kuzalisha umeme wa uhakika, kuendesha viwanda, kutumika majumbani na hata kwenye usafiri kupitia miundombinu ya kisasa ya mabomba na vituo vya kujaza gesi. Hii siyo tu itashusha gharama za maisha kwa Mtanzania wa kawaida, bali itatengeneza ajira za kumwaga na kulinda mazingira yetu kwa kishindo.
Wale wanaopenda "kupiga domo" na kubeza juhudi hizi, sasa ni wakati wa kunyamaza kwa aibu. Tanzania imeshajichanganya kimataifa, imejipambanua kama kitovu cha nishati, na sasa rasilimali zetu zinaanza kuleta matunda yatakayobadilisha maisha ya kila mwananchi. Mama Samia ameshika mpini, na nchi inasonga mbele kuelekea utajiri wa kutisha!
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464