Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, akizungumza wakati wa hafla ya ugawaji wa vitendea kazi kwa TANESCO Mkoa wa Shinyanga iliyofanyika Ijumaa Machi 27, 2026 mjini Kahama.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 Blog
Serikali kupitia Wizara ya Nishati imekabidhi vitendea kazi kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Shinyanga, ikithibitisha dhamira yake ya kusogeza huduma za umeme karibu na wananchi na kuimarisha utendaji wa taasisi zake ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Vitendea kazi vilivyokabidhiwa ni pamoja na magari manne, bajaji moja, na pikipiki mbili, vitakavyotumika kuboresha utoaji wa huduma za umeme, hasa katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji.
Hafla ya makabidhiano imefanyika leo Ijumaa, Machi 27, 2026, mjini Kahama, ambapo Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, amebainisha umuhimu wa uwekezaji katika sekta ya nishati.
“Lengo la serikali ni kuhakikisha huduma ya umeme inawafikia wananchi wote, iwe ni mijini au vijijini. Uboreshaji wa miundombinu pamoja na kuwapatia watumishi vitendea kazi bora ni sehemu ya mkakati wa kutoa huduma haraka, yenye ufanisi na kwa gharama nafuu”, amesema Mhe. Makamba.
Aidha, Mhe. Makamba amewahimiza wananchi kuanza kutumia majiko ya umeme, hatua itakayosaidia kuhamasisha matumizi ya nishati safi, salama kwa afya, na rafiki kwa mazingira.
Ameongeza kwamba matumizi ya nishati safi yatachochea kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa, hivyo kupunguza uharibifu wa mazingira na hatari za kiafya.
Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Benson Nasania Mbigili, amesema vitendea kazi hivyo vitasaidia kufikia maeneo mengi na kuboresha utoaji wa huduma za umeme kwa wananchi, huku akisisitiza kuwa vifaa hivyo ni nyenzo muhimu za kuharakisha kazi za TANESCO na kufanikisha malengo ya taifa katika sekta ya nishati.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa vitendea kazi kwa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, katika hafla iliyofanyika leo Ijumaa Machi 27, 2026 mjini Kahama. Vitendea kazi vilivyokabidhiwa ni pamoja na magari, bajaji na pikipiki vitakavyosaidia kuimarisha huduma za umeme kwa wananchi. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa vitendea kazi kwa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, katika hafla iliyofanyika leo Ijumaa Machi 27, 2026 mjini Kahama. Vitendea kazi vilivyokabidhiwa ni pamoja na magari manne, bajaji moja na pikipiki mbili vitakavyosaidia kuimarisha huduma za umeme kwa wananchi.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, akijaribu kuendesha moja ya magari yaliyokabidhiwa kwa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, wakati wa hafla ya ugawaji wa vitendea kazi iliyofanyika Ijumaa Machi 27, 2026 mjini Kahama.

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, akijaribu kuendesha Bajaji iliyokabidhiwa kwa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, wakati wa hafla ya ugawaji wa vitendea kazi iliyofanyika Ijumaa Machi 27, 2026 mjini Kahama.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, akijaribu kuendesha moja ya pikipiki iliyokabidhiwa kwa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, wakati wa hafla ya ugawaji wa vitendea kazi iliyofanyika Ijumaa Machi 27, 2026 mjini Kahama.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba (wa kwanza kulia), akisikiliza maelezo kutoka kwa afisa wa TANESCO kuhusu matumizi ya majiko ya umeme (nishati safi ya kupikia), wakati wa hafla ya ugawaji wa vitendea kazi kwa TANESCO Mkoa wa Shinyanga iliyofanyika Ijumaa Machi 27, 2026 mjini Kahama.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba (wa pili kulia), akisikiliza maelezo kutoka kwa afisa wa TANESCO kuhusu matumizi ya majiko ya umeme (nishati safi ya kupikia), wakati wa hafla ya ugawaji wa vitendea kazi kwa TANESCO Mkoa wa Shinyanga iliyofanyika Ijumaa Machi 27, 2026 mjini Kahama.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, akipokea zawadi kutoka TANESCO wakati wa hafla ya ugawaji wa vitendea kazi kwa TANESCO Mkoa wa Shinyanga iliyofanyika Ijumaa Machi 27, 2026 mjini Kahama.

Muonekano wa sehemu ya magari yaliyokabidhiwa kwa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, katika hafla ya ugawaji wa vitendea kazi iliyofanyika Ijumaa Machi 27, 2026 mjini Kahama, kwa ajili ya kuimarisha huduma za umeme kwa wananchi.

Muonekano wa baadhi ya magari, bajaji na pikipiki zilizokabidhiwa kwa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, katika hafla ya ugawaji wa vitendea kazi iliyofanyika Ijumaa Machi 27, 2026 mjini Kahama, kwa lengo la kuimarisha na kuongeza ufanisi wa huduma za umeme kwa wananchi.

Muonekano wa sehemu ya magari yaliyokabidhiwa kwa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, katika hafla ya ugawaji wa vitendea kazi iliyofanyika Ijumaa Machi 27, 2026 mjini Kahama, kwa ajili ya kuimarisha huduma za umeme kwa wananchi.
Muonekano wa sehemu ya magari yaliyokabidhiwa kwa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, katika hafla ya ugawaji wa vitendea kazi iliyofanyika Ijumaa Machi 27, 2026 mjini Kahama, kwa ajili ya kuimarisha huduma za umeme kwa wananchi.
Muonekano wa sehemu ya magari yaliyokabidhiwa kwa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, katika hafla ya ugawaji wa vitendea kazi iliyofanyika Ijumaa Machi 27, 2026 mjini Kahama, kwa ajili ya kuimarisha huduma za umeme kwa wananchi.

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, akizungumza wakati wa hafla ya ugawaji wa vitendea kazi kwa TANESCO Mkoa wa Shinyanga iliyofanyika Ijumaa Machi 27, 2026 mjini Kahama, akisisitiza umuhimu wa kuimarisha miundombinu ya umeme na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Benson Nasania Mbigili, akizungumza kwenye hafla ya ugawaji wa majiko ya umeme na vitendea kazi, iliyofanyika Ijumaa Machi 27, 2026 mjini Kahama ambapo amesema vitendea kazi vilivyokabidhiwa vitasaidia kufikia maeneo mengi na kuboresha utoaji wa huduma za umeme kwa wananchi, wakati wa hafla iliyofanyika Ijumaa Machi 27, 2026 mjini Kahama.
Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Benson Nasania Mbigili, akizungumza kwenye hafla ya ugawaji wa majiko ya umeme na vitendea kazi, iliyofanyika Ijumaa Machi 27, 2026 mjini Kahama

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, akimkabidhi mwananchi zawadi ya jiko la umeme baada ya kujibu kwa usahihi maswali kuhusu huduma za TANESCO, wakati wa hafla ya ugawaji wa vitendea kazi iliyofanyika Ijumaa Machi 27, 2026 mjini Kahama.

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, akimkabidhi mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kahama ambaye ni Katibu Tawala Wilaya ya Kahama, Gloria Absalom jiko la umeme wakati wa hafla ya ugawaji wa vitendea kazi iliyofanyika Ijumaa Machi 27, 2026 mjini Kahama.
Mkazi wa Kahama akisoma shairi mbele ya hadhira wakati wa hafla ya ugawaji wa vitendea kazi kwa TANESCO Mkoa wa Shinyanga iliyofanyika Ijumaa Machi 27, 2026.

Katibu Tawala Wilaya ya Kahama, Gloria Absalom akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kahama. Thomas Muyonga, akizungumza kwenye hafla ya ugawaji wa vitendea kazi kwa TANESCO mjini Kahama, Shinyanga, Machi 27, 2026.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kahama, Mhe. Kaniki Mataruma, akizungumza kwenye hafla ya ugawaji wa vitendea kazi kwa TANESCO mjini Kahama, Shinyanga, Machi 27, 2026.

Mchekeshaji maarufu, Headmaster, pamoja na kikundi chake, wakizungumza na hadhira wakati wa hafla ya ugawaji wa vitendea kazi kwa TANESCO Mkoa wa Shinyanga iliyofanyika Ijumaa Machi 27, 2026 mjini Kahama.
Picha za pamoja.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog