` MTANDAO WA POLISI WANAWAKE MKOANI SHINYANGA WAADHIMISHA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI

WANDAMAN HOTEL

MTANDAO WA POLISI WANAWAKE MKOANI SHINYANGA WAADHIMISHA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI

               Na Mwandishi wetu kutoka Wilayani Kahama.

Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Shinyanga TPF–NET umeitaka jamii kupinga vitendo vya ukatili kwa watoto wote wa kike na wa kiume bila ubaguzi ili kulinda usalama wa watoto na kuimarisha haki zao licha ya kuwa hali hiyo itasaidia kutatua changamoto ya kuporomoka kwa maadili .

Wito huo umetolewa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika katika kata ya Mondo wilayani Kahama Mkoani Shinyanga na viongozi mbalimbali wa Jeshi la polisi .

 Viongozi hao ni pamoja na SP. Ester Zefania OCD (W) Kishapu, SP Flora Nangawe Mkuu wa Usalama Barabarani (W) Kahama na ASP Zainab Mangala OCD (W) Shinyanga wametoa elimu kwa wananchi juu ya kupinga ukatili wa kijinsia wakisisitiza watoto wakiume kutazamwa kwa umakini kwakuwa ukatili dhidi yao umekuwa ukiongezeka.

Aidha baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Shinyanga akiwemo Zawadi Athuman na Ernest Isumbi wamesema vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vimepungua kwa kiasi kikubwa baada ya Jeshi la Polisi kuimarisha ushirikiano na wananchi hali inayosababisha kasi ya kuripoti matukio ya uhalifu kuongezeka.

Kaimu Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Shinyanga SSP Fatuma Mitarimbo amesema kuna umuhimu jamii kupinga ukatili kwa watoto wote wa kike na wa kiume bila kujali kwa kuwa kampeni nyingi zimekuwa zikilenga zaidi mtoto wa kike pekee huku watoto wakiume wakisahaulika na kuenelea kuingia katika wimbi la maporomoko ya maadili.

Aidha amewasisitiza wanaume kuhakikisha wanashriki katika masuala mazima ya malezi na makuzi ya watoto wao kwakuwa ni jukumu la wazazi wote.






















Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464