` WANANCHI SHINYANGA WAITWA KUHUDHURIA MKUTANO MKUBWA WA INJILI KUPOKEA UPONYAJI VIWANJA VYA SABASABA

WANDAMAN HOTEL

WANANCHI SHINYANGA WAITWA KUHUDHURIA MKUTANO MKUBWA WA INJILI KUPOKEA UPONYAJI VIWANJA VYA SABASABA

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

WANANCHI wa mkoani Shinyanga wameitwa kujitokeza kwa wingi kudhuria mkutano mkubwa wa injili utakaofanyika kwa siku nne kuanzia leo hadi Jumapili, ambapo pamoja na mambo mengine utaombea amani ya Tanzania.

Mkutano huo unafanyika katika viwanja vya sabasaba ambao  utahusisha maombi kwa wananchi wenye matatizo mbalimbali ikiwamo magonjwa, pamoja na kutoa huduma ya maombezi na msaada kwa watu wenye uhitaji.
Akizungumza na waandishi wa habari Machi 12,2026 Rais wa huduma ya Nuru kwa Mataifa na Muinjilisti wa Mkutano huo Dana Morey kutoka Marekani, amesema katika siku hizo nne watatoa huduma ya maombezi kwa wagonjwa, kusaidia watu wenye uhitaji pamoja na kuombea amani ya Tanzania.

“Mwili wa Yesu Kristo upo tayari kuwahudumia wananchi wa Shinyanga, tunawaomba wajitokeze kwa wingi kupokea huduma ya uponyaji, na siku ya mwisho ya mkutano huu tutaombea amani ya Tanzania,” amesema Morey.
Mwenyekiti wa mkutano huo Mchungaji Seleman Joseph wa Kanisa la TAG Shinyanga, amesema maandalizi yote ya mkutano yamekamilika, na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki.

Amesema, mkutano huo utatoa fursa kwa watu kupokea wokovu na maombezi ya uponyaji ili waweze kuishi maisha yenye furaha na amani.

TAZAMA PICHA👇👇
Rais wa huduma ya Nuru kwa Mataifa na Muinjilisti wa Mkutano mkubwa wa Injili ambao unafanyika mkoani Shinyanga Dana Morey akizungumza na waandishi wa habari.

Mwenyekiti wa mkutano wa Injili mkoani Shinyanga Mchungaji Seleman Joseph wa Kanisa la TAG Shinyanga akizungumza.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464