
Waumbe wa baraza la wazazi wilaya ya Shinyanga mjini wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumaliza kikao chao
Suzy Butondo, Shinyanga press blog
Viongozi wa Jumuiya ya wazazi kuanzia matawi kata na wilaya katika wilaya ya Shinyanga mjini, wametakiwa kuendelea kusikiliza kero za wananchi ili kupunguza changamoto mbalimbali kwenye jamii.
Hayo yamesemwa leo na katibu wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Dorice Kibabi kwenye kikao cha baraza kilichofanyika leo mjini hapa,ambapo ameyasema haya wakati akisoma taarifa ya jumuiya hiyo.
Kibabi amesema jumuiya ya wazazi toka mwezi Januari ilielekezwa kusikiliza kero mbalimbali za wananchi mpaka Decemba mwaka huu ili kupunguza changamoto mbalimbali zilizopo kwenye jamii.
"Mpango mkakati wa wazazi ni kuimarisha jumuiya ya wazazi, na kila kata inatakiwa kuwa na kiwanja pamoja na miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuendelea na zoezi la usajili kwa wanachama wote ili kuhakikisha kila mwanachama anasajiliwa kwenye jumuiya ya wazazi"amesema Kibabi.
Kwa upande wake katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga Said Bwanga amewaomba viongozi wote washirikiane kwa pamoja katika kufanya kazi zote za Jumuiya na CCM, waachane na makundi ya uchaguzi yaliyokuwepo wawe wamoja ili kuhakikisha kazi za jumuiya na chama zinafanyika kama kawaida.
"Nawasihi tuache makundi tushirikiane kwa pamoja katika kutatua kero za wananchi katika kata zote, na tunapokutana na kero tuzipeleke kwenye chama ili ziweze kutatuliwa kwa wakati"amesema Bwanga.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Fue Mrindoko amewapongeza viongozi wote wajumuiya ya wazazi kwa kusimamia uchaguzi, na kupata ushindi wakishindo, hivyo amewaomba waendelee kushirikiana na kuwa na umoja.
"Niwaombe sana wajumbe wangu haya yote tuliyokumbushana tukayafanyie kazi na kuhakikisha tunayatekeleza ni jukumu letu wazazi kusikiliza kero za wananchi,pia twendeni tukaanzishe miradi mbalimbali katika maeneo yetu ili tuweze kuwa na kitega uchumi, nizipongeze kata zote ambazo tayari zina viwanja niwaombe nawengine ambao bado tuwe na viwanja ambavyo vitatusaidia kujenga na kufanya miradi "amesema Mrindoko
Katibu wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga mjini Dorice Kibabi akitoa taarifa kwa wajumbe wa baraza
Katibu wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga mjini Dorice Kibabi akizungumza na wajumbe wa baraza
Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga mjini akizungumza na wajumbe wa baraza
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464
