` MWENYEKITI CCM MKOA WA SHINYANGA MABALA MLOLWA AWATAKA UWT KUJIEPUSHA NA MIGOGORO

MWENYEKITI CCM MKOA WA SHINYANGA MABALA MLOLWA AWATAKA UWT KUJIEPUSHA NA MIGOGORO

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, ameitaka Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) CCM mkoani humo, wawe na mshikamano, umoja, upendo, na kujiepusha na migogoro inayoweza kudhoofisha Jumuiya hiyo.

Ametoa nasaha hizo leo Februari 20, 2026 wakati akifugua kikao cha baraza la hilo la UWT.
Amesema, wanawake ni Jeshi kubwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ameshaonyesha njia kwa utendaji wake kazi uliotukuka katika kuwatumikia wananchi, na hivyo kuwasihi wanawake hao wa UWT wasimame imara, washikamane wawe wa moja na wenye upendo, na siyo kuwa na migogoro, ili waimalishe Jumuiya yao na kukijenga Chama.

“Uchaguzi umeisha, sasa mnapaswa muwe na mshikamano, umoja, upendo na msiwe na migogoro, fanye kazi kama timu moja,” amesema Mabala.
Aidha, amewapongeza pia Madiwani wanawake ambao walishinda kwenye Kata, pamoja na Wabunge na kuwashinda wanaume, na kuwasihi nafasi hizo wazitumikie vizuri, pamoja na kufanya mikutano ya hadhara kutatua kero za wananchi.

Naye Mwenyekiti wa UWT, Mkoa wa Shinyanga Grace Bizulu, amesema kikao hicho cha baraza ni muhimu, kwa ajili ya kuimarisha umoja wao na kukijenga chama.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Nishati Salome Makamba ambaye ni Mbunge wa Vitimaalum mkoani Shinyanga kupitia UWT, na Mjumbe wa Jumuiya ya Maendeleo ya Mataifa ya Kusini mwa Afrika SADC Mwanahamisi Munkunda.

TAZAMA PICHA👇👇
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza.
Mwenyekiti wa UWT CCM Mkoa wa Shinyanga Grace Bizulu akizungumza.
Katibu wa UWT Mkoa wa Shinyanga Habiba Musimu akizungumza.
Naibu Waziri wa Nishati Salome Makamba akizungumza.
Mjumbe wa Jumuiya ya Maendeleo ya Mataifa ya Kusini mwa Afrika SADC Mwanahamisi Munkunda akizungumza.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464